Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
Dk. Maria Kamm akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kuibuka kinara wa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/14.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia Nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niaba ya Dk. Asha-Rose Migiro, Anne Kilango Malecela, Dk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.
Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na washindi, waandaaji wa tuzo hizo kutoka Global Publishers Ltd.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo, akitoa hotuba fupi wakati wa utoaji tuzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Mama Magreth Sitta (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ester Bulaya (kulia) wakifuatilia zoezi la utoaji tuzo.
DK. Maria Kamm ametwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 baada ya kuwapiku wenzake watatu jana usiku.
Dk. Kamm ametwaa tuzo hiyo baada ya kupata asilimia 32.5 ya kura zote zilizopigwa kupitia tovuti ya www.globalpublishers.info pamoja na meseji kupitia simu za mikononi.
Mshindi wa pili alikuwa Dk. Asha-Rose Migiro aliyejizolea jumla ya asilimia 30 ya kura zote, wa tatu Profesa Anna Tibaijuka akiwa na asilimia 20 na wa nne Anne Kilango Malecela mwenye asilimia 17.5 ya kura zilizopigwa kwa wanawake hao wanne walioingia Nne Bora.
Washidi wote wanne walipewa tuzo japo mshindi wa kwanza alijipatia medali pamoja na shilingi milioni tano.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Mkoani Dodoma, Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda aliyetoa tuzo hizo.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL, DODOMA)