Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi... Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya). Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Mkuu wa Kijiji... Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Wageni waalikwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea... ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
Mshindi wa Maisha Plus 2012, Beneriki (wa kwanza kulia) akifuatilia uzinduzi huo. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Waandishi wa habari waliofika kuhudhuria tukio hilo wakishow love. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi... washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka... wengine walitamani kughairi kuendelea na safari. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wengine ilibidi wasaidiane kupeba mizigo. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe... Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Washiriki wakiwa wameamua kupumzika baada ya kuona safari yao ya kuzisaka shilingi milioni 25 imekuwa ni ndefu. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
WASHIRIKI wa mashindano ya Maisha Plus rekebisha, jana wameingia Kijijini katika eneo ambalo lipo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mshindi wa mashindano hayo kwa mwaka huu anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni 25. Katika mashindano hayo jumla a washiriki 29 wameingia katika Kijiji hicho.
Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika jana, Mkurugenzi wa mashindano hayo, Ally Masoud ‘Kipanya’, alisema kuwa washiriki hao wametokea kwenye nchi za Afrika Mashariki.
Alisema kuwa mchujo wa washiriki hao, unatarajiwa kuanza baada ya wiki mbili.
Alisema kuwa washiriki hao wametokea kwenye nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania.
Alisema kuwa washiriki hao walipewa masaa 48 kwa ajili ya kujenga nyumba ambazo wataziumia.
Alisema kuwa pia washiriki wa mashindano ya Mama Shujaa wa Chakula wanatarajiwa kuwasili wiki mbili za mwisho ambapo washiriki wa Maisha Plus Rekebisha wanatarajiwa kukaa kwa muda wa siku 60.
“Mashindano ya mwaka huu yatakuwa tofauti na yale yaliyopita, na hivyo tunatarajia yatakuwa ya kuvutia zaidi, na washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula wataingia katika wiki mbili za mwisho” alisema.