Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ACCESS BANK YAFUNGUA TAWI LA 10, TABORA

$
0
0
Mwakilishi wa Uongozi wa AccessBank Tanzania Emmanuel Venance akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari hawapo pichani wakati wa ufunguzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo mkoani Tabora. Tawi hilo lilifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Fatma Abubakar Mwassa (wa tatu kutoka kulia) mnamo tarehe 15/3/14. Wengine katika picha ni Afisa Masoko Mkuu Mwandamizi wa Benki hiyo Ndugu Muganyizi Bisheko (Pembeni ya Mkuu wa mkoa) na wa kwanza kushoto ni mmojawapo kati ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Fatma Abubakar Mwassa akikata utepe kuzindua rasmi tawi la AccessBank Tabora mnamo tarehe 15th March 2014. Wa kwanza kutoka kushoto ni Afisa Masoko mkuu mwandamizi wa benki hiyo Ndugu Muganyizi Bisheko akifatiwa na muwakilishi wa uongozi wa AccessBank Ndugu Emmanuel Venance. Waliosimama kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tabora mh. Suleiman Kumchaya akifatiwa na Meneja wa Tawi hilo ndugu Enosy Ndobeji
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Fatma Abubakar Mwassa akitoa hotuba yake katika uzinduzi wa Tawi jipya la AccessBank mkoani Tabora likiwa ni tawi la kumi tangu Benki hiyo kuanzishwa mnamo mwaka 2007.

Meneja wa Tawi la AccessBank, Tabora ndugu Enosy Ndobeji akitoa neno la shukrani kwa walioudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi hilo. Kushoto kwake ni Afisa Masoko mkuu mwandamizi wa Benki hiyo ndugu Muganyizi Bisheko na aliekaa kulia ni Mwakilishi wa uongozi wa Benki hiyo ndugu Emmanuel Venance.
Wafanyakazi wa AccessBank tawi la Tabora wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hili iliyofanyika tarehe 15th March 2014.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>