Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TIGO YATOA MSAADA WA VITABU VYENYE THAMANI YA MIL. 6 KWA SHULE YA MSINGI KILIMANI, DAR

$
0
0

  Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael akiwakabidhi msaada wa vitabu, Happiness Mathias (kushoto) na Ibrahim Issa, wanafunzi wa shule ya Kilimani, iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam mapema leo. Akishuhudia katikati yao ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Zubeda Jeni. Tigo ilikabidhi msaada wa vitabu 905 vyenye thamani ya milioni 6.1 na tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 kwa shule hiyo.
 Mratibu wa Elimu wa kata ya Manzese Bi. Petronila Liyamuya (kulia) akipitia moja ya vitabu vilivyokabidhiwa na Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael (kushoto) mapema leo katika shule ya msingi Kilimani, Manzese. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Kilimani Bi. Zubeda Jeni.
  Mwalimu Mkuu wa shule ya Kilimani iliyopo Manzese Bi. Zubeda Jeni (kushoto) akimshukuru Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael kwa msaada wa tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 yenye thamani ya Tsh 653,000/- pesa iliyochangishwa na wafanyakazi wa Tigo.
 Risala ikisomwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kilimani Bi. Zubeda Jeni ambapo aliishukuru kampuni ya simu Tigo kwa msaada wa vitabu na tenki la maji iliyotolewa. Mwalimu mkuu huyo alisema msaada huo uliotolewa ni kitendo cha kizalendo kilichofanywa na anaamini kwamba vitabu hivyo vitaongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi walio darasa la nne na la saba wataonufaika moja kwa moja na msaada huo.
Wafanyakazi wa Tigo katika picha ya ukumbusho na wanafunzi na walimu wa shule ya Kilimani iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam. Tigo ilifika mapema leo kutoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 6.1 pamoja na tenki la kuhifadhia maji yenye uwezo wa kubeba lita 4000.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles