Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TIGO YADHAMINI MPANGO WA KUPUNGUZA AJALI ZA BODA BODA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Tigo Tanzania imetangaza kushirikiana na taasisi ya usalama wa pikipiki nchini katika kuzindua Mpango wa Huduma Salama ya Usafiri wa Bodaboda Kitaifa itakayofanyika mjini Dodoma, 23 Machi, 2014.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, iliyowashirikisha pia wakala wa usalama wa pikipiki nchini (TAMOSA), Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha, alisema kwamba udhamini wa Tigo katika mpango huo wa kitaifa wa usalama wa bodaboda nchini ni ishara ya kwamba kampuni hiyo ya simu inajalina kufuatilia kwa karibu kuhusu masuala ya usalama barabarani nchini.

“Wote ni mashuhuda wa jinsi biashara hii ya pikipiki ilivyoweza kushamiri ndani ya muda mfupi nchini. Kupitia bodaboda na bajaji vijana wetu wameweza kujiajiri wenyewe na kuweza kujipatia kipato kinachowasaidia kumudumaisha,”alisemaWanyancha.

“Lakini kila kitu huja na changamoto zake, na katika hili suala la ajali barabara nilimekuwa dosari kubwa. Kama kampuni, tuliamini kwamba hiii takuwa fursa nzuri kwa sisi kama wadau kujaribu kuhamasisha kuhusu usalama barabarani kwa ajili ya kusaidia kupunguza idadi ya ajali zinazotokea huku tukihakikisha kwamba sekta hii inaendelea kuwachachuya ajira kwa vijana nchini,”alisema.

Kutokana na maelezo ya Mratibu wa Matukio kutoka TAMOSA, Kizito Msangya, alisema kwamba uzinduzi wa mpango huo wa usalama utafanyika kwa njia ya maandamo ya amani kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa mpaka Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ndio atakuwa mgeni rasmi.

“Tunatarajia mamia ya wamiliki na waendesha pikipiki kutoka nchini kote kufika katika tukio hili. Ukiondoa mbali na Mheshimi wa Pinda, pia tunatarajia Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, wabunge pamoja na mamlaka za usalama barabarani kushiriki katika uzinduzi huu,”alisema Msangya.

Ripoti za Polisi zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio 264 ya ajali barabarani kwa mwaka 2013 sawa na asilimia 1.1 tofauti na mwaka 2012 ambapo matukio yalikuwa 23,578.

Takwimu pia zinaonyesha kuwa walioathirika zaidi na ajali za barabarani kwa mwaka 2013 ni waenda kwa miguu, abiria, waendesha pikipiki, wapanda baiskeli, madereva pamoja na wasukuma mikokoteni.
 Ambapo kati ya makundi hayo, ajali za pikipiki zimeongoza kwa ajali nyingi, kwa mwaka 2013 ajali zilikuwa 6,831 sawa na ongezeko la asilimia 18.5 ya ajali 5,763 zilizotokea mwaka juzi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>