Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

WATANZANIA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KATIKA UWEKEZAJI

$
0
0
Afisa Mahusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bi. Pendo Gondwe (katikati) akiongea na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, juu ya shughuli zinazofanywa na kituo hicho ikiwemo changamoto na mafanikio waliyoyapata tokea kituo kimeanzishwa. Pembeni mwake kushoto ni Meneja uhamasishaji wa Kituo hicho, Bw. John Mnali na Afisa Habari idara ya habari maelezo, Bw. Frank Mvungi.
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
Meneja uhamasishaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mnali akisistiza jambo  wakati wakiongea na waandishi wa habari. Pembeni mwake ni Afisa Mahusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bi. Pendo Gondwe na  Afisa Habari idara ya habari maelezo, Bw. Frank Mvungi.
---
TIC inapenda kutoa taarifa kwa Watanzania kuhusu mwamko na ushiriki wa Watanzania katika kuchangamkia fursa za Uwekezaji hapa nchini ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ili kuongeza kipato chao na kuinua uchumi wa Taifa letu.

Kama sehemu ya jukumu letu, TIC ina jukumu la kuhamasisha uwekezaji na masuala yanayohusiana na Uwekezaji kwa Watanzania ili Uwekezaji uweze kuwa na manufaa kwa nchi Watanzania kwa ujumla.
Kutokana na uhamasishaji wa uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani, Idadi ya miradi ya uwekezaji inayomilikiwa na watanzania imekuwa ikiongezeka kila mwaka na hadi kufikia Desemba mwaka jana asilimia 52 ya miradi iliyowekezwa ilikuwa inamilikiwa na watanzania. Wakati asilimia 25 ilikuwa ya ubia na asilia 23 ni ya wageni.

Baadhi ya sekta mbalimbali ambazo tunahamasisha usajili wa miradi kwa Watanzania ni Kilimo na ufugaji, Maliasili, Utalii, Viwanda, Madini, Usafirishaji, TEKNOHAMA, Umeme, Elimu, Afya, Miundo mbinu n.k. Hivyo watanzania wana uhuru wa kuamua ni sekta gani wangependa kuwekeza.

Kituo cha Uwekezaji (TIC) kwa muda mrefu tumekuwa tukihamasisha watanzania washiriki kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya Uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. Kutokana na juhudi za Kituo cha uwekezaji pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali, tumeweza kuwavutia watanzania wengi ambao ni wafanya biashara kuweza kuanzisha miradi ya uwekezaji kwenye sekta ambazo zimetajwa hapo juu.

Hata hivyo bado tunaamini kuwa kuna watanzania wengi ambao wana uwezo wa kuanzisha miradi ya uwekezaji na wengine wameanzisha lakini bado hawajasajiliwa na Kituo cha Uwekezaji. Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba watanzania kutumia huduma za Kituo cha Uwekezaji wanapoamua kuanzisha miradi yao ya uwekezaji.

Kituo cha Uwekezaji (TIC) kinatoa huduma mbalimbali kwa ajili ya wawekezaji wa ndani kupitia dirisha moja yaani “ONE STOP CENTRE” kama ifuatavyo;-
1. Kuandikisha Kampuni
2. Kujisajili na VAT, TIN
3. Leseni mbalimbali
4. Hati za ukazi daraja ‘B”,endapo utahitaji kumwajiri mgeni
5. Ushauri wa bure kuhusu kodi
6. Usaidizi wa kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji
7. Vivutio vya uwekezaji
8. Kuunganishwa na wawekezaji wan nje kwa ajili ya ubia
9. Usaidizi wa kutafuta masoko kupitia ziara za nje za wafanyabiashara wa Tanzania.

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha watanzania wote kuwa Kituo cha Uwekezaji (TIC) kipo kwa ajili yao na huduma hizi zinapatikana kwa wale wanaozihitaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zetu tembelea kwenye tovuti yetu ambayo ni www.tic.co.tz.

Mwisho, kutokana na mchango wa wawekezaji wa ndani kwenye uchumi wa nchi yetu, Kituo Cha Uwekezaji (TIC) kimetenga kitengo maalum kwa ajili ya kuwasaidia wawekezaji wa ndani. Hivyo, tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha watanzania wote kutumia huduma zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>