Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TIGO NGORONGORO MARATHON KUCHANGISHA PESA KWA AJILI YA KUPAMBANA NA MALARIA

$
0
0
Mwaka wa saba wa ‘Tigo Ngorongoro Half Marathon’ iliyopewa kauli mbiu ya “Kimbia kuikabili Malaria” itafanyikaJumamosiya 19 Aprili 2014 wilayani Karatu, jijini Arusha. 

Mbio hizo za kila mwaka inategemea kuwavutia wanariadha 3,000 wa kitaifa na kimataifa, Tigo ilitangaza leo.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha, alisema kwamba Tigo Ngorongoro Marathon ni fursa ya kuhamasisha jamii kuhusu jinsi ugonjwa wa Malaria unavyoathiri watu milioni 300 mpaka 500 duniani, asilimia 90 wakiwemo barani Afrika.

“Malaria inaua zaidi watu milioni moja kila mwaka. Nchini Tanzania mtu mmoja anafariki kwa ugonjwa wa malaria kila baada ya dakika 10. Mbio za mwaka huu inahusisha pia harambee ya kujenga kituo cha hospitali,” alisema Wanyancha.

Mwaka wa 7 wa mbio hizi za Tigo Ngorongoro Half Marathon inaambatana na maadhimisho ya Siku ya Malaria inayoadhimishwa tarehe 25 Aprili kila mwaka. Tukio hilo, kutokana na maelezo ya Wanyancha inategemewa kuzinduliwa na Waziriwa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu kama mgeni rasmi.

Tigo inashirikiana na moja ya makampuni ya utalii yanayoongoza nchini kwa jina la Zara Tanzania Adventures, katika kuandaa mashindano haya, ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kununua na kugawa neti za mbu, pamoja na kununua dawa za malaria ambapo zitagawiwa mahospitalini Arusha bure.

Fedha zitakazochangishwa pia mwaka huu zitatumika kukarabati vituo vya afya vilivyopo pamoja na kujenga kituo kipya cha afya kitakachoanzishwa Ngorongoro pamoja na shule ya awali katika vijiji tofauti tofauti kwa gharama ya shilingi milioni 160 jumla, alisema Wanyancha.

“Mbio za Tigo Ngorongoro half marathon sio tu burudani kwa watu watakaoshuhudia bali ni sehemu nzuri sana yenye kuhamasisha kuhusu namna ya kujikingana kutibu ugonjw wa malaria kwa jamii inayozunguka maeneo ya Monduli na Arusha kwa ujumla,” alisema.

Mbio hizi zinawapa fursa wanariadha kukimbia katika sehemu moja yenye vivutio vya kipekee duniani, kutoka kivutio cha Ngorongoro mpaka jiji la Karatu. Mbio za mwaka huu pi aina husishama shindano ya makampu ni ya kilomita 5 kwa makampuni wenye nia yakuchangia katika harambee hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles