Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi hundi kwa washindi watatu waliopewa dola 25,000 kila mmoja chini ya mradi wa Tigo Reach for Change.
Tigo leo imechagua na kutangaza washindi watatu watakaopewa dola 25,000 kila mmoja chini ya mradi wa Tigo Reach for Change uliozinduliwa mwezi Novemba mwaka jana yenye malengo ya kuboresha maisha ya watoto nchini.
Wajasiriliamali jamii hao watatu walioshinda ni:
1.Faraja Nyalandu, na mradi wa Shule Direct;
‘Shule Direct’ ina malengo yakuhamasisha na kuhakikisha kwamba mtaala bora ya elimu inapatikana kidigitali kiurahisi na kwa ufanisi zaidi kupitia njia ya simu za mkononi (SMS na kwa kupiga) kwa ajili ya maendeleo mema ya wanafunzi wakitanzania.
2. Joan Avit na mradi wa GraphoGame Tanzania;
‘GraphoGame’ ni mchezo wa watoto uliowekwa kwenye mfumo wa kompyuta (apps) inayoweza kutumika kwa njia ya simu yenye malengo ya kuwawezesha watoto kujua kusoma na kuandika. Imewekwa kwa njia ya mchezo ili kuweza kuwa fanisi zaidi kwa kuwafurahisha na kuwashirikisha watoto pindi wanapokuwa wanajifunza.
3. Carolyne Ekyarisiima na mradi wa Apps and Girls;
‘Apps and Girls’ ina malengo ya kuwahamasisha wasichana na wanawake kuweza kuelimika zaidi katika masuala ya Teknohama.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman akielezea jinsi walivyoendesha zoezi la kuchagua mawazo yaliyotumwa na watu zaidi ya 1000.
“Kutoa huduma za kijamii ni moja kati ya nguzo kuu katika kampuni yetu, na tumejikita sana katika mradi huu ambao ni mpango maalum ndani ya mitandao wetu duniani kote. Tigo Tanzania imepokea miradi mizuri mengi sana na tumeweza kufanya mchujo mkali sana. Washindi watatu walioshinda siku ya leo hawakuwafurahisha tu jopo la majaji waliokamilisha zoezi hili bali majaji walipima na kuona kwamba miradi yao yana mantiki na yenye uwezo kiukweli kukabili matatizo ya watoto. Washindi hawa watakuwa wanapokea dola 25,000 kila mmoja kwa mwaka kwa muda wa miaka mitatu kwa ajili ya kukamilisha malengo ya miradi yao,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga.
Aliendelea kusema, “Ushirikiano wa Tigo Reach for Change una malengo ya kutambua na kuwawezesha wajasiriliamali jamii wenye mawazo yakibunifu yenye uwezo wa kuboresha maisha ya watoto nchini Tanzania. Washindi hawa watatu wataingizwa rasmi kwenye mpango maalum wa miaka mitatu ambao utawawezesha wajasiriliamali jamii hao kupata ushauri kutoka kwa wataalam wetu ya namna bora ya kuendesha mradi yao. ”
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. Woinde Shisael akitangaza washindi wa shindano la Tigo Reach for Change.
Novemba mwaka jana, Tigo ikishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Reach for Change ilizindua kwa mara ya pili mradi wenye malengo ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasirialamali jamii ambao wangekuja na miradi mizuri na yakibunifu yenye uwezo wa kuboresha maisha ya watoto mchini.
“Baada ya kukaribisha maombi ya mradi kwa muda wa mwezi mmoja, tulipokea maombi 1,100, ambapo 15 ndio walioweza kutinga fainali baada ya mchujo mkali sana kufanyika na ulioendeshwa na wafanyakazi wa Tigo na Reach for Change, pamoja na msaada wa wataalam kutoka nje. Wanafainali hawa waliweza kutetea miradi yao mbele ya jopo la majaji ambao nao walivikwa na jukumu zito la kuchagua washindi watatu tu kati ya hao,” alisema Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman.
Reach for Change ni asasi isiyo ya kiserikali kutoka nchini Sweden ambayo ilianzishwa na kampuni ya Kinnevik, kampuni mama ya Millicom. Zoezi la kuwatafuta wajasirialamali jamii lilianza kwa mara ya kwanza nchini Sweden mwaka 2010, ikifuatiwa na Urusi 2011, kabla ya kufanya majaribio pia barani Afrika katika nchi ya Ghana katika mwaka huo huo. Ghana hivi karibuni walitoa ripoti inayoonesha kwamba mradi huo umeweza kuboresha maisha ya watoto wapatao 140,000.
Tigo na Reach for Change walianza rasmi kutafuta wajasirialamali jamii katika nchi zote wlizowekeza Afrika kutoka Agosti mwaka 2012 kwa kuzindua mradi wake wa kwanza nchini Rwanda, ikifuatiwa na Tanzania, halafu Congo DRC, Ghana, Chad na mwisho Senegal.
Meza Kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Reach for Change nchini Tanzania na Rwanda, Richard Gorvett, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Bw. Eduardo Quiroga pamoja na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. Woinde Shisael wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga, akikabidhi mfano wa hundi ya dola 25,0000 za Kimarekani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Bi. Faraja Nyalandu (kushoto) kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar leo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman.
Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Bi. Faraja Nyalandu akionyesha mfano wa hundi hiyo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga, akikabidhi mfano wa hundi kwa Mshindi wa mradi wa GraphoGame Tanzania, Joan Avit (kushoto) kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar leo.Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman.
Mshindi wa mradi wa GraphoGame Tanzania, Joan Avit mwenye furaha akionyesha mfano wa hundi hiyo kwa waandishi wa habari.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Reach for Change Bw. Jacob Stedman(katikati) akikabidhi mfano wa hundi kwa Mshindi wa mradi wa Apps and Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Eduardo Quiroga.
Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Bi. Faraja Nyalandu akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa hundi ya dola 25,0000 za Kimarekani iliyotolewa chini ya mradi wa Tigo Reach for Change.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo.