Katika pita pita za Kajunason Blog ndani ya Mitandao ya Kijamii kusikia wadau wanalizungumziaje Bunge Maalum la Katika ilikutana na ujumbe ambao ulipata wachangiaji wengi ambao waliliponda na kusema ni bora Mh. Rais Jakaya Kikwete aweze kulivunja maana hao aliowatuma kufanya kazi wanamuaibisha kwa kauli na vitendo vyao wanavyovifanya ndani ya bunge hilo.
Vile vile wananchi walisema wanakerwa kuona watu hao wanapokea posho kila kukicha lakini mpaka sasa imeshafika siku 22 ila hakuna kinachoendelea.
UJumbe wa mwananchi huyo katika ukurasa wake wa facebook ulisema hivi, 'KWAKWELI KAMA NINGEKUWA RAIS NINGELIFUTILIA MBALI HILI BUNGE, KAMA NINGEKUWA NA MUME WANGU AMETEULIWA KUSHIRIKI NINGEMUOMBA ARUDI DAR'
Maoni ya wachangiaji yalikuwa kama ifuatavyo;-
Mwananchi 1. KAMA KARIAKOOOO EEEHHH???HAHAHAHHA BUNGE LIMEJAA WAHUNI WATUPU.
Mwananchi 2. Hahahaha ndugu yangu umeona utumbo wanaoufanya enhe, mi kitambo nilishawaona mburulazzzzzzzzzzz.
Mwananchi 3. Kama wa mashabiki wa timu fulani ya pale maji machafu dah! hadi mzee wangu Ole nae vurugu hatari! ila jioni account inasoma dada.
Mwananchi 4. Duh! Nafikiri Rais angetengua uteuzi wa watu wengine. Baadhi ya watu wengine kule adabu imewapita kushoto.
Mwananchi 5. Kwa upande wangu mimi naumia sana, kiukweli umeona mbali.. Hawa ni mafisadi wanaokula kodi zetu wananchi bure.
Mwananchi 6. Unalolizungumzia kwa wenye akili timamu na upeo mkubwa wa kufikiri na kuona mambo yanavyokwenda, lazima wawe upande wako, haiingi akilini watu wazima kama wale walioaminiwa na mh. rais kwenda kuitengeneza katiba wawe wanafanya mambo kama yalee, hapana ule ni upuuzi na ujinga lazima upingwe kwa nguvu zote.