Mrembo wa Tanzania Happiness Watimanywa pamoja na Mkurugenzi wa Bang magazine Bi. Emelda Mwamanga wakiwa na kina mama wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo cha kigamboni(Chawawaki) kwenye sherehe ya siku wanawake Duniani, ambayo iliandaliwa na taasisi ya wanawake wenye mafanikio Tanzania TWA.
Mshauri nasaha na mtoa mafunzo wa ccbrt Bi. Mgaya Mhamanda akiongea na kinamama wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo cha kigamboni(Chawawaki) kwenye sherehe ya siku wanawake Duniani, ambayo iliandaliwa na taasisi ya wanawake wenye mafanikio Tanzania TWA.
Katibu wa kikundi cha Chawawaki Bi. Upendo Ikombe katikati akiwa na Miss Tanzania Happiness Watimanywa(kushoto) na Bi. Grace Rubambeyi mshindi wa tuzo za Twaa, kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani zilizofanyika shule ya msingi Mji Mwema Kigamboni.
Kina mama wa kikundi cha Chawawaki Kigamboni wakimsikiliza rais wa Taasisi ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania TWA Bi. Irene Kiwia (hayupo pichani) kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani yenye lengo la kusaidia kikundi hicho.
Mrembo wa Tanzania Happiness Watimanywa akikabidhi baiskeli kwa mwenyekiti wa Chawawaki Bi. Reberata Jovin kwenye sherehe zenye lengo la kusaidia kikundi hicho, ambazo zimeandaliwa na taasisi ya TWA.