Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MKUU WA MKOA WA DSM AWATAKA WAKAZI WA JIJI LA DAR KUHAMA MABONDENI

$
0
0

Na Aron Msigwa –MAELEZO, Dar es Salaam.

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Meki Sadiki amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan wale wanaoishi katika maeneo hatarishi yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara kutii taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kuondoka katika maeneo hayo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.

Akitoa taarifa kuhusu mikakati ya kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea wakati wa msimu wa mvua kama ilivyotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Mh. Meck Sadiki ameeleza kuwa tayari serikali imejipanga chini ya kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwa na kikosi kazi kinachohusisha vikosi vya ulinzi na usalama vya majeshi ya Tanzania.

Ameeleza kuwa serikali kwa kuthamini umuhimu wa maisha ya raia wake hasa wale waishio mabondeni imekuwa ikitoa taarifa za kuhama mapema lakini baadhi yao hugoma kuyahama maeno yao na pindi wanapoondolewa kwa nguvu huamua kwenda mahakamani kuishitaki serikali.

“Mara nyingi tumekuwa tukiwataka mara kwa mara wale wote wanaoishi bondeni kuhama sio tu wakati wa msimu wa mvua lakini wenzetu wamekua wakiona suluhisho lao ni kukimbilia mahakamani jambo ambalo linasababisha mahakama kusimamisha zoezi letu kama tunavyojua serikali yetu inaheshimu uhuru wa mahakama”

Kuhusu kesi zilizopelekwa mahakamani kuhusiana na zoezi la kuwaondoa wananchi wanaoishi katika bonde la mto Msimbazi amesema tayari kuna kesi nne zinazoendelea kushughulikiwa na tayari Manispaa ya Ilala imeshinda kesi moja.

Ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki ikiwemo kutoa taarifa za matukio yanayohatarisha maisha na kujenga tabia ya kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza pia kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapoona baadhi ya watu wanajenga katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles