Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma Machi 6, 2014 baada ya Bunge hilo kusitihwa kwa muda kufuatia Sitofahamu iliyotokea. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Katika hali ya sintofahamu Mwenyekiti wa Muda wa Bunge maalum La Katiba Mh. Pandu Kificho Ameahirisha bunge hilo Kutokana na Vuruguru Kutokana na Hali ya Kutokuelewana Kati ya Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mheshimiwa Ole Sendeka Kutoleana maneno na Mbunge Mwenzake wakati Mbunge Huyo alipohoji kuhusu Kanuni hizo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa muda Machi 6,2014 kufuatia sintofahamu ilitokea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).