Baadhi ya magari yaliyoangukiwa na ukuta.
Gari aina ya Noah likiwa limegandamizwa na zege.
Hali ilivyokua tete katika zahama hiyo ya alfajiri ya leo.
Muonekano wa Magari mbalimbali yakiwa chini ya kifusi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.
Sehemu ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo.
Ukuta wa eneo la ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal umeangukia magari zaid ya 24 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo bajaji tatu,yaliyokuwa yamepaki eneo ambalo hutumika kupaki wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeelezaa kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa akibomoa ukuta huo, na pia imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.
Baadhi ya Maofisa kutoka Jeshi la Polisi wakiangalia baadhi ya magari yaliyoathiriwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta mapema leo asubuhi kwenye eneo la kupaki magari, ndani ya kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani. Ukuta huo ulikuwa ukibomolewa na Mkandarasi ikiwa ni hatua za awali wa kituo hicho kuvunjwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi.
Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
Si Magari tu, hata bajaji pia zimeathiriwa vibaya kama uonavyo pichani.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Afande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi
Mmoja wa watu,ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliyeathiriwa na tukio hilo pichani kati akiwa amezungukwa na Maofisa wa jeshi la Polisi, akielezea namna hali ilivyokuwa. Picha na Michuzijr Blog.