Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YAKUTANA NA WADAU WA SEKTA MBALI MBALIKUJADILI UTABIRI WA MVUA ZA MSIMU KWA MWEZI MACHI-MEI (MASIKA)

$
0
0
NA MONICA MUTONI; OFISI YA UHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA​​
Kila mwaka mwezi Februari kabla ya kutoa utabiri wa msimu Mamlaka hukutana na wadau wa sekta mbali mbali nchini ili kujadili utabiri wa msimu huo wa mvua za MASIKA kwa kipindi cha miezi ya Machi hadi Mei na kuwapa wadau nafasi ya kuchangia namna utabiri huo utakavyotumika katika sekta zao.

Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi alisema mchango wa wadau katika matumizi ya utabiri ni wa muhimu kwani utabiri unaotolewa hauwezi kuwa na manufaa endapo wadau kutoka sekta mbalimbali hawatautumia katika kuboresha shughuli zao.Aliongeza kusema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hali ya hewa imekuwa ikibadilika sana (climate variability) hivyo akasisitiza kwamba ni muhimu sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii zikatilia maanani taarifa za hali ya hewa katika mipango ya shughuli zao.

Mshiriki kutoka Wizara ya Kilimo na usalama wa chakula (MAFS-NFRA) Bw. Joseph Peter Oganga alieleza umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta mbalimbali hususan kwenye upatikanaji wa chakula kwa kupanga namna ya kutumia utabiri katika kupanga uzalishaji wa mazao husasn katika kipindi hiki ambacho dunia nzima ikishuhudia mabadiliko ya tabia nchi .

Mshiriki kutoka Timu ya Wataalamu wa Kukabiliana na Maafa Mkoa wa Dar es salaam – DARMAERT(Dar es salaam Multi-Agency Emergency Response Team) Bw. Amini Mshana kwa upande wake alisema mikutano hii inasaidia sana kujiandaa na maafa ili kupunguza athari zinazoletwa na maafa akitolewa mfano mafuriko,mlipuko wa magonjwa n.k

Kwa upande wa sekta ya habari, Mwakilishi kutoka Magic radio Bw Salum Mkambala alisema wanahabari ndio kiunganishi cha jamii hivyo ni muhimu kujua changamoto zinazoikabili TMA katika usambazaji wa taarifa za hali ya hewa na kutafuta muafaka huku wakitumia fursa hii kuwaomba wadau wengine kutoa taarifa zinazoeleweka kwa kila mwana jamii hususan zile zitokanazo na hali ya hewa

Taarifa za hali ya hewa ni muhimu katika sekta ya afya kwani magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ni mengi kama vile malaria na kuharisha, alisema mshiriki kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bw. Makono Andrew.

Wadau walioshiriki na kutoa michango yao katika mkutano huo ni kutoka Wizara ya Afya (MNCP) Makono Andrew na Amina Kingo (Epidemiology), Wizara ya Maji Mwasiti Rashid, Wizara ya Mifugo Lugendo Bunto,RedCross, TBC Mwasu Sware, Salum Mkambala (Magic FM),DARMEART Amini Mshana, Wizara ya Uchukuzi Shinja Shaffih, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa DSM Boniface Chija, Ofisi ya Mipango Josiah Mwabeza, Wizara ya Kilimo Joseph Ogonga, Wizara ya Nishati na Madini Innocent Makomba, Climat Consult Philbert Tibaijuka, Ofisi ya Waziri Mkuu (maafa) Edward Boniface, CWCAR-DSM Dkt Mohamed Mhita

Akifunga mkutano huo Dkt. Agnes Kijazi alisema utabiri wa msimu wa MASIKA utatolewa rasmi tarehe 27 Februari 2014.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>