Wabunifu ‘Lady in red’ Februari 14 hadharani
..Wamo magwiji: Ally Remutulla, Mustapha Hassanal, Khadija Mwanamboka, Martin Kadinda
..Chipukizi wamo Faustin Simon, Water Edward,Willex Willibard, Jackson, Alabama King
Na Mwandishi Wetu, Dar
WABUNIFU mbali mbali watakaopamba miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari 14, tayari majina yao yamewekwa hadharani. Onyesho la mwaka huu linatarajia kufanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam, Februari 14, huku asilimia ya mapato ya fedha hizo zinatarajia kusaidia wathirika wa dawa za kulevya wa kituo cha Kikale Kilichopo Mkoani Pwani.
Akiongea na wandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo, Asia Idarous Khamsin, alisema kila mwaka onyesho hilo huja kitofauti ikiwemo kuongeza vionjo mbalimbali katika kufikia mafanikio kwenye tasnia ya ubunifu na mitindo ya mavazi hapa nchini.
“Safari hii, steji ya Lady in red’, inatimiza miaka 10, huku ikijivunia kuibua vipaji vya wabunifu wengi hapa nchini, na wengine kwa sasa wanamajina makubwa kwenye yasnia hiyo, hivyo tutaendelea kutoa nafasi kwa wabunifu chipukizi mara kwa mara ilikufikia malengo yao” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous aliwataja wabunifu magwiji watakaopamba steji hiyo kuwa ni pamoja na Khadija Mwanamboka, Mustapher Hasanal , Ally Remtulla, Lucky Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali, Paka wear, Gabriel Molel, Fransiska Frankoo, Shirima, Salim Ally, Ameed Abdul, Mgese Makory, Kiki Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine.
Kwa upande wa wabunifu chipukizi watakaopamba ni pamoja na Faustin Simon, Water Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Uissoson,Willex Willibard, Jackson, Gumbala, Jabir Jumanne, Alabama King, Agusta Masaki, Nelson Tomas, Bebi Juliet Mtandu, Ummi fashion/Ummi Investiment Comapany, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru, Ante Ngongi, Adam Hassan, Jaquline, Kijangwa na Waiz Shelukindo.
Aidha, Asia Idarous aliongeza kuwa, kwenye onyesho tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza kuuzwa ikiwemo vituo vya duka la Fabak fashion, lililopo mikocheni mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena, zikipatikana mapokezi.