Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MASHINDANO YA NGARAWA YAFANA TANGA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), kizindua mashindano ya Ngalawa Wilayani Muheza.
Ngalawa zikiwa katika mstari kwa ajili ya kuanza mashindano katika pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.
---
Na Mwandishi Wetu, Muheza

Mashindano ya ngalawa yaliyofanyika jana Wilayani Muheza katika Kijiji cha Kigombe yamefana.

Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo amewataka vijana washiriki katika michezo badala ya kukaa vijiweni.

Kauli hiyo aliitoja wakati akifungua mashindano ya kwanza ya Ngalawa mkoani Tanga yaliyofanyika kwenye Pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.

Mwidau alisema kupitia michezo vijana wataweza kupata fursa nyingi ikiwemo elimu na ujunzi kutoka kwa wenzao ,burudani pamoja na kujenga afya za kimwili na kiakili.

“Mahindano haya ya Ngalawa hapo awali yalikuwa yanafanyika ngazi ya kijiji lakini tumeweza kuyafanya kimkoa kwa lengo la kuibua fursa za ajira kwa vijana na kwashirikisha watu katika michezo, ”alisema Mwidau.

Mshindi wa kwanza alijipatia kitita cha Shilingi laki tatu, kikombe cha ushindi pamoja na medali za dhahabu.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka ambaye aliweza kujinyakuliwa zawadi hiyo.

Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya Ngalawa thelathini zilizokuwa na washiriki watano ambapo washiriki walitoka katika Wilaya za Tanga, Pangani na Muheza huku Wilaya ya Mkinga ikishindwa kushiriki kutokana na kushindwa kufanya maandalizi mazuri.




Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>