Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TIGO YADHAMINI KIJANA MTANZANIA AMBAYE NI MWENDESHA BAISIKELI DUNIANIKATIKA KUKUZA UELEWA WA MAZINGIRA NA KUTOA MSAADA WA KIFEDHA KWAWANAOJIENDELEZA NA ELIMU YA JUU

$
0
0

Tigo Tanzania leo imetanganza udhamini na uwezeshaji wake kwa Elvis (lelo) Munis, huyu ni mwendesha baisikeli kijana kabisa wa kitanzania mwenye ari kubwa, ambaye amekuwa akiendesha baisikeli duniani kote kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita katika kujaribu kutunisha mfuko wa ufadhili kwa wanafunzi wa kitanzania 10 ili kuleta uelewa juu ya uhifadhi wa mazingira.

Munis, ambaye ni kijana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 27 mzaliwa wa mkoa wa Kilimanjaro, kupitia uwezeshaji uliofanywa na kituo cha utunzaji wa maliasili, alianza kuizungukia dunia chini ya mradi unaoitwa Chile to kili” ambapo anategemea kupata dola za kimarekani 100,000 ili kuwasaidia wanafunzi wa kitanzania wenye ujuzi, uelewa na ari wenye kuonyesha nia kubwa katika usimamizi wa wanyamapori katika nchi yetu ya Tanzania,lakini hawana uwezo wa kifedha ili kujiendeleza na elimu ya juu.

Kupitia maelezo yaliyotolewa kwenye vyombo vya habari leo, Meneja masoko wa Tigo bwana William Mpinga alisema “ kampuni ya tigo inafuraha kubwa sana kumdhamini kijana huyu aliyejitolea muda wake na nguvu zake kwa malengo mazuri kwa jamii yake pia na kwa nchi yake.

Maliasili ndio akiba ya kesho ya taifa letu; kutengeneza ujuzi wa kutunza rasilimali hizi ni muhimu sana katika kuhakikisha ukuaji wa uchumi endelevu. Tunawaalika watanzania duniani kote kujumuika katika juhudi hizi kwa kumtumia mchango kupitia tigo pesa 0716407057’. Tigo Tanzania imetoa kiasi cha dola za kimarekani 10,000 ili kumsaidia kijana munis katika maisha yake, nauli za hapa na pale na gharama zinginezo.

Ingawa mpinga alisema, Tanzania ina kila aina ya wanyamapori, mazingira mazuri na ina sehemu nyingi zenye urithi mkubwa duniani, but watu wake wengi hawana rasiliamali fedha, msukumo na motisha wa kupata elimu ambayo ni muhimu katika kuwezesha, kuendeleza na kuhifadhi hizi maliasili.

Tuna furaha kubwa sana kuona Tigo wamekuja kutusaidia katika kufikia malengo yetu, alisema kijana Lelo Munis.

Mpinga alisema fedha itakayopatikana katika mpango huu itatolewa kwa wanafunzi ambao wanataka kujiendeleza na elimu yao ya ngazi ya cheti, shahada ya kwanza au shahada ya kuhitimu kozi katika uhifadhi wa wanyamapori, usimamizi wa rasilimali, ikolojia au fani yoyote inayoendana na maswala haya chini ya usimamizi wa kituo cha uhifadhi wa rasilimali. Kituo hiki huwa kinasaidia uhifadhi, kwa kutoa elimu za kitaaluma, na huduma mbalimbali kwa wanafunzi na watafiti wa kitanzania.

Kwa upande wake Mshauri wa kituo cha ufihadhi wa rasilimali, bwana Howard Fredrick alisema, taasisi yake inaona fahari kutoa msaada kwa mwendesha baisikeli huyu kama fursa ya kusaidia vijana wengi wa kitanzania kutimiza ndoto zao katika uhifadhi wa mazingira

“Wakati Lelo alipokuja katika kituo chetu cha CRC miaka michache iliyopita na dhana yake ya kutoka Chile mpaka Kilimanjaro, tulijua angelishinikiza kwa msukumo mkubwa tu suala hili na lingefanikiwa, na sisi baada ya yeye kuonyesha nia hiyo tuliingiwa na msisimko wa kusaidia.

Tunaona wanafunzi wengi sana kila mwezi hapa kwenye kituo chetu, wengi wao wanatafuta njia za namna gani wajiendeleze katika elimu zao ili kufanya kazi katika kuhifadhi na kutunza urithi wa rasilimali zetu. Mradi huu wa Chile to Kili’ moja kwa moja utawasaidia wanafunzi hawa wanaotaka kujiendeleza. Kwa hiyo tunawahimiza kila mmoja kusaidia katika mradi huu.” Alisema Fredrick katika maelezo yake.

Safari ya Lelo ameanzia Chile, Argentina, Bolivia, Brazil, Colombia, Mexico, USA, Canada, Norway, Sweden, Denmark, German, Holland, Belgium, France, UK, Luxembourg, Spain, Portugal, Morocco, Western Sahara, Mauritiana na sasa yuko senegali na kuanzia hapa ataendesha kuelekea Guinea Bissau, Guinea Conakry, Liberia, Sierra Leone, Ivory Coast, Ghana, Togo, Benin, Nigeria, Cameroon, Gabon, Equatorial Guinea, Congo Brazzaville, Congo Kinshasa, Burundi, and na hatimaye kufika katika vilima vya mlima Kilimanjaro katikati ya mwezi wa sita mwaka huu 2014.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>