Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MWANZA HOI, CHEPE CHEPE MVUA INAPONYESHA

$
0
0
Mifereji ya maji taka ni finyu nayo ikishinda bila kufanyiwa usafi ikiwa ni pamoja na uzibuaji hali huwa tete.

Adha waipatayo wafanyabiashara waliopangisha kwenye maduka ya majengo yaliyopo pembezoni kwa kituo cha daladala za Mwaloni zamani karibu na soko kuu. Mitaro imejaa, barabara zimejaa maji, Si biashara tena bali sasa ni kila mmoja kuokoa mali zake.

Ili kuepuka kadhia hii ambayo kama mvua ingenyesha nyakati za usiku ingekuwa hasara kubwa kwa mali zilizowekwa sakafuni, basi ni jukumu sasa la kila mfanyabiashara kuhakikisha takataka za maboski, mifuko, vitambaa na bidhaa nyingine za kutupa, kuwa zinahifadhiwa kwenye mapipa maalum ya taka na si kuyaelekeza kwenye mifereji ya maji taka.

Picha zote na Gsego Blog.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles