Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKAMILISHA ZOEZI LA KUWANOA WAKUFUNZI WAUTAFITI WA WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI

$
0
0
Wakufunzi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa sekta ya Elimu Wariambora Nkya (hayupo kwenye picha) aliyefunga mafunzo ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendela

Picha zote na John Nditi).
---
Na Veronica kazimoto – Morogoro

Viongozi wote wa Serikali katika ngazi zote kwa ujumla wameombwa kutoa ushirikiano katika kuhamasisha na kuelimisha umma umuhimu wa kushirikiana na Wadadisi pamoja na Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi unaotarajia kuanza rasmi mwezi Februari na kumalizika Disemba mwaka 2014.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Morogoro Wariambora Nkya wakati akifunga Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Edema mkoani Morogoro.

Nkya amefafanua kuwa ni muhimu viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wasimamizi kwani utafiti huo ni muhimu katika kuboresha sera na program mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA.

"Nitoe wito kwa viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano kwa Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 ili waweze kutekeleza majukumu yao kama ilivyopangwa", amesema Nkya.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa sekta ya Elimu, Wariambora Nkya, (wapili kutoka kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014, mara baada ya kufunga mafunzi hayo, jana kwenye ukumbi wa Edema, Mjini Morogoro ( wapili kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo.

Wakati huo huo Katibu Tawala Nkya amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano wa kujibu maswali na kutoa taarifa sahihi wakati watafiti watakapopita katika makazi yao kukusanya taarifa za soko la ajira katika ngazi ya Kaya.

"Napenda kuwahakikishia Wananchi kwamba shughuli zao za kiuchumi na kijamii hazitasimamishwa na zoezi la Utafiti huu kwa kuwa Wadadisi watakusanya takwimu za Utafiti huu wakati shughuli zingine zikiedelea kama kawaida", amesisitiza Nkya.

Wariambora Nkya ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera na mafunzo hayo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu yamemalizika ambapo jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini walihudhulia mafunzo hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>