Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TIGO YATOA SHILINGI MILIONI 400 KWA WATEJA WAKE

$
0
0
Nuru Staford, mkazi wa Tabata ambaye ni mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Tigo 'Shinda kitita na Tigo Pesa' akipokea mfano wa hundi ya Sh. milioni 2 kutoka kwa Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta leo jijini Dar es Salaam. Kufikia leo Tigo imeshatoa jumla ya shilingi milioni 400 kwa wateja wake 1,215 waliokwisha shinda na promosheni hii.
Mkazi wa Tazara, Nassoro Yusuphu, mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Tigo 'Shinda kitita na Tigo Pesa' akipokea mfano wa hundi ya Sh.Milioni 2 kutoka kwa Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta leo jijini Dar es Salaam. Bado shilingi milioni 720 zimebakiwa kushindaniwa ndani ya mwezi mmoja uliobaki katika promosheni hii.
Shabani Omary, mkazi wa Temeke ambaye ni mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Tigo 'Shinda kitita na Tigo Pesa' akipokea mfano wa hundi ya Sh.Milioni 2 kutoka kwa Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta leo jijini Dar es Salaam. Zaidi ya shilingi bilioni 1.12 zitashindaniwa mpaka mwisho wa promosheni hii katikati ya mwezi Februari 2014.
Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni washindi wa droo ya tatu ya Tigo 'Shinda kitita na Tigo Pesa' Nassoro Yusuphu (kushoto) na Nuru Staford.
---
Tigo imekabidhi jumla ya zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 400 ndani ya mwezi mmoja katika promosheni yake ya ‘Cheza Kwa Furaha Unaposhinda Kitita na Tigo Pesa’ huku fedha zingine 720 milioni zikibakia kushindaniwa.

Akizungumzia muenendo wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Mary Rutta alisema kwamba jumla ya zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya bilioni 1.12 zitashindaniwa na watumiaji wa Tigo Pesa mpaka pale promosheni hiii itapofikia ukomo katikati ya mwezi wa Februari.

Rutta alisema tayari wateja 1,215 kutoka kila mkoa nchini ameweza kujishindia zawadi hizi akiongeza, “tunatarajia idadi kubwa zaidi ya wateja wa Tigo Pesa kushinda katika mwezi unaokuja ya kampeni yetu ambayo bado jumla ya shilingi milioni 720 zimebakia kushindaniwa.”

“Tunaendelea kutoa wito kwa wateja wetu wa Tigo kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa kadri wawezavyo katika muda huu uliobaki wa promosheni ili waweze kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda,” alisema Rutta.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa pia alikabidhi zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 110 kwa washindi wengine 375 walioshinda kwenye droo ya promosheni hiyo wiki iliyopita, ambapo washindi 20 walijishindia shilingi milioni 2 kila mmoja na wengine 350 pia walijinyakulia shilingi laki 2 kila mmoja.

Washindi watatu waliokuwepo katika makabidhiano hayo walisema kwamba wamefurahi sana kushinda fedha hizo taslimu na kuahidi kwamba watatumia fedha hizo kuboresha maisha yao.

Anachohitaji kufanya mteja ili kuingia kwenye droo, alisema Rutta, ni kutumia akaunti yake ya Tigo Pesa kutuma fedha, kununua bidhaa, kuongeza salio au kulipia bili mbali mbali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>