Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Amani katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo mchana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na usalama, wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Amani, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mjini yaliyofanyika leo.
Viongozi wa Serikali na viongozi waalikwa, wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na baadhi ya viongozi waalikwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, wakati alipokuwa akiwasili uwanja wa Amani leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akikagua gwaride maalum la sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo mchana.
Askari wa zamani wanaoigiza gwaride la enzi za ukoloni, 'Tarabush' wakipita mbele ya jukwaa kuu na kuonyesha jinsi askari hao walivyokuwa wakicheza gwaride hilo, wakati waa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar. Picha na OMR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Vijana wakiachia njiwa kama alama ya amani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein wakimpongeza Rais Yoweri Kaguta Museveni aliyeongea machache wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein kwa hotuba nzuri aliyotoa wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
PICHA NA IKULU