Mbunge Amina Mwidau, akimkabidhi kikombe cha ushindi Nahodha wa timu ya APL Mwera Shabani Athuman, baada ya timu hiyo kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Mwidau CUP, mjini Pangani leo
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akihutubia kabla ya kuchezwa kwa fainali kati ya timu ya APL Mwera na Torino (kulia) ni Katibu wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, Salehe Swazi.Mgeni rasmi katika Mashindano ya Mwidau CUP, Amina Mwidau akijadiliana na viongozi wenzake wakati wa mchezo wa fainali ya Mwidau CUP kati ya APL Mwera dhidi ya Torino leo mjini hapa.APL Mwera yaibuka kidedea Mwidau CUP
---
Na Mwandishi Wetu, Pangani
TIMU ya Soka la APL kutoka Kata ya Mwera, imetoka kifua mbele huku wakitangazwa mabingwa wapya wa kombe la Mwidau CUP.
Timu hiyo iliibuka na ushindi dhidi ya timu ya Torino ya mjini Pangani, ambayo ilishindwa kufua dafu kwa kufungwa kupitia penati.
Hadi dakika tisini za mchezo huo wa fainali hiyo ya Mwidau CUP zinamalizika timu zote zilishindwa kutambiana na kulazimika kutoka suluhu ya bao 1-1.
Kutokana na hali hiyo timu hizo ilizilazimu kuingia katika hatua ya matuta ambap kati ya penati nne zilipingwa kwa kila timu, Torino ilipoteza penati mbili huku APL Mwera ilipoteza moja hali hiyowafanya kuibuka na ushindi na kutawazwa mabigwa wa ligi hiyo.
Timu hizo hadi zinakwenda mapumziko katika kipindi cha kwanza kila timu ilitoka huku ikishindwa kuona nyau ya mwenzake lakini ilipofika dakika ya 57, mchezaji Christopher Gunda wa APL alifanikiwa kuziona nyavu za Torino.
Hata hivyo katika dakika ya 62 Torini ilijibu mapigo na kusawazina bao hilo ambapo hadi dakika 90 timu zote zilishindwa kutambiana na kuamua kupigwa matuta.
Awali akihutubia kabla ya kuanza kwa mchezo huo mgeni rasmi katika mashinda hayo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), aliwataka vijana kuthamini michezo kwani ajira ambayo imekuwa na manufaa kwa Taifa.
“Kwa imani yangu ninaamini hata hapa Pangani tunao wachezaji wazuri kupitia timu zetu hizi zilizoshiriki ligi hii ya Mwidau CUP ambao wana uwezo wa kufanya vizuri katika timu kubwa za ndani na nje ya nchi yetu,” alisema Mwidau.