Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

KASEBA NA USHINDI WA MAGUMASHI DHIDI YA ALIBABA, MASHABIKI WATAMPONZA

$
0
0
 Bondia Japhet Kaseba, akitangazwa mshindi baada ya pambano hilo kuvunjika katika raundi ta tano.
 Japhet Kaseba (kushoto) na Alibaba, wakichapana ulingoni.

Na Sufianimafoto.com
MARA kadhaa mapambano ya ngumi ya aliyewahi kuwa Bingwa wa mchezo wa Kick Boxer nchini, aliyehamia katika ulingo wa masumbwi, nchini Japhet Kaseba, yamekuwa hayamaliziki kutokana na mizengwe ama vurugu zinazosababishwa na mashabiki wake ukumbini. 

Kaseba aliwashawahi kupigana na Francis Cheka siku za nyuma katika pambano lao lililofanyika katika uwanja wa Uhuru, na pambano hilo lilivunjika kutokana na vurugu zilizoanzishwa na mashabiki, ambao haikuweza kufahamika walikuwa ni Cheka au Kaseba.

Lakini sasa inaonekana kumekuwa na muendelezo wa matukio kama hayo katika mchezo huu, ambayo nahisi yamekosa dawa na udhibiti wa uhakika kutoka kwa waandaaji, ambao nao sina uhakika sana kama wanashindwa kuwadhibiti watu kama hao kutokana na miundombinu ya kumbi zetu za mchezo huu au ni kujipanga.




Kwa haiingii akilini kwamba 'Eti shabiki wa bondia flani atoke atokako', asogee hadi katika ulingo na kufanya afanyalo kwa mpinzani wa bondia wake, wakati kuna walinzi waliowekwa kudhibiti watu wasiohusika wasisogee eneo la ulingo zaidi ya wasaidizi wa mabondia. 




Ama nao pia huwashobokea waandishi wa habari tu ili waonekana wanafanya kazi au kujitafutia umaarufu kwa kuwazuia waandishi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao na kuwaacha wanaostaihili kudhibitiwa.
Bondia Alibaba, akiwa chini baada ya kuchapwa konde zito na mpinzani wake Kaseba katika raindi ya pili.

Mara kadhaa unaweza kukuta mwandishi anavielelezo vyote vinavyomfanya kuingia ama kusogea mahala flani kwa kutekeleza kazi yake lakini anazuiliwa, huku wasiohusika wakiachiwa tena bila hata kuulizwa jambo wala kusumbuliwa na matokeo yake ndo kama hayo yaliyotokea jana katika pambano la ngumi la Kaseba na Alibaba.







Katika pambano hilo lililokuwa la Raundi 10, Kaseba alitangazwa mshindi baada ya pambano hilo kuvunjika katika raundi ya 5, wakati Alibaba alipoamua kususia pambano hilo na kuvua Gravz zake na kutupa chini, akilalamika kwa mwamuzi wa kuwa amefanyiwa visivyo na shabiki wa mpinzani wake, aliyemshika mguu na kumpotezea 'timming' na kutaka kuanguka huku akishushiwa makonde ya mfululizo na mpinzani wake hadi ilipopigwa kengele.

Ni kweli Alibaba alikuwa na haki ya kulalamika katika hili, kwani Kaseba alionekana kuanza kuzidiwa katika raundi ya tatu jambo lililomfanya shabiki huyo ambaye alionekana na kila mtu aliyekuwa karibu kusogea pembeni mwa ulingo na kumshika mguu, Alibaba na kumvuruga hadi kushindwa kuendelea na pambano hilo, huku vurugu ikizuka ukumbini mashabiki wa pande zote mbili wakianza kurushiana chupa za maji na kuwafanya watazamaji wengi kutimua mbio ukumbini humo kujinusuru.


''Waandaaji wa mapambano ya ngumi, tujifunze kutokana na makosa na ikiwezekana tuwe wabunifu wa kuandaa taratibu zitakazofanya mchezo huu uweze kuendelea na kuzidi kupendwa chini kuliko kuzidi kuchukiwa na watu kutokana na matukio kama hayo, kwani wanakuja kupata burudani hii si wote wenye uwezo wa kumudu vurugu''.

''Kaseba akiendelea na michezo yake ya kihuni kama hii kamwe hawezi kuendelea, na atapoteza mashabiki wake kibao tu''. alisikika mmoja wa mashabiki waliokuwa wakitoka ukumbini humo kwa hasira akilalama

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>