Ankal akimkabidhi zawadi ya Krismasi na kadi Kamanda wa FFU Ughaibuni The Ngoma Africa Band ya Ujeruman, Ras Ephraim Makunja, a.k.a Field Marshal wa jamii ya Annunaki walipokutana leo katikati ya jiji la Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya faragha ya saa moja katika kiota cha Break Point cha mjini. Katika mazungumzo yao waliongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuendeleza undugu uliopo baina ya Globu ya Jamii na FFU Ughaibuni, na kupanga tarehe ambazo The Ngoma Africa Band itakuwa huru kuja kufanya maonesho kadhaa nchini Tanzania.
Ras Makunja anarivenji kwa kumkabidhi Ankal zawadi ya moja ta T-Shirt kibao alizomletea zikiwa na logo ya Globu ya Jamii.
Ankal akimshukuru Ras Makunja kwa zawadi hiyo mwanana
Ras Makunja akiwa na mjomba wake akijiondoa eneo la tukio taratibu huku kakumbatia zawadi yake ya Krismasi na kadi. Meno yote arobaini yako nje kwani hakutegemea kupata heshima hii. Picha kwa hisanio ya mpiga picha wa The Ngoma Africa Band aliyeongozana naye katika ziara hii ya mapumziko jijini Dar es salaam. Mara ya mwisho kufika Bongo kwa Ras Makunja ilikuwa miaka sita iliyopita, na ameshangazwa na mabadiliko na maendeleo makubwa aliyotaona kila mahali, kuanzia nyumbani kwake mtaa wa Aggrey ambako mbavu za mbwa yao imeshajengwa bonge la Ghorofa, nusura apotee, na huko kwake Segerea ambako anasema kuna lami mpaka jikoni....