Muonekano wa ndege ya Ethiopian Airline baada ya kutua kwa dharura.
Watu 200 waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Ethiopian Airline wanusurika kufa baada ya ndege kupitiliza hadi nje ya uwanja mdogo wa ndege wa Arusha baada ya kutua kwa dharura.
Picha Kwa Hisani ya DJ SEK BLOGNdege aina ya Boeing 767 inayosadikiwa kuwa ni ya Shirika la Ndege la Ethiopia imetua kwa dharura majira ya saa tisa alasiri katika kiwanja cha kurushia ndege ndogo cha Arusha badala ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, KIA.