Kwa kawaida Kajunason Blog ilikuwa ikikuletea Utalii wa Ndani katika maeneo mbali mbali ambayo hupata fursa ya kutembelea na kujionea mambo mbali mbali yakiwemo yale ya historia ya zamani. Wikendi iliyopita nilipata fursa ya kutembelea mji wa Kilwa Masoko na kujifunza mambo mbali mbali. Ila moja ya kitu nilichojifunza ni kuwa usafiri unaopendwa na watalii toka nje ni wa ndege ambapo ukiangalia ukuta wa matangazo utakuonyesha sehemu ambazo zinatembelewa zaidi kwa kila siku.
Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa kituo muhimu ya biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 BK Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.
Katika karne ya 14 -kati ya 1330 na 1340 BK- mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya kwanza ya kimaandishi kuhusu mji. Majengo makubwa yalijengwa ikiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama vile msikiti kuu, nyumba ya kifalme ya Husuni Kubwa na mengi mengine.
Kilwa Masoko ni mji mdogo katika Tanzania ikiwa makao makuu ya Wilaya ya Kilwa tangu miaka ya 1960.
Iko barani ikitazama Kilwa Kisiwani. Mji ni wa kisasa. Kuna uwanja mdogo wa ndege pia bandari ndogo yenye kituo cha forodha. Kata ina wakazi 12,324
Ndege hizi ukizikuta uwanja wa zamani wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama daladala za Mwenge-Posta ambapo kila baada ya nusu saa kuna zinazofika na nyingine kuondoka na msululu wa watu ni mkubwa.
Ndege zikiwa tayari kwa safari za kila siku katika uwanja wa zamani wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Wafanyakazi nao wapo busy kuendelea na shughuli zao.
Marafiki zangu James Range (kulia) na Hemed nilioambatana nao katika safari yangu ya Kilwa kupitia Kisiwa Cha Mafia.
Nikifurahia jambo na rafiki yangu James Range... wakati tunaelekea kupanda pipa.
Acha niende zangu....
Kila mmoja alikuwa busy... kuelekea kupanda pipa.
Pipa likiwekwa sawaaaa....
Ndani ya pipa la watu 11...
Muonekano wa Mji wa Dar unavyoonekana kwa juu...
Nilipata wasaa wa kuweka kumbukumbu na rafiki yangu James...
Muonekano wa mji wa Kilwa kwa pembezoni mwa bahari ya hindi...
Uoto wa Asili ndani ya Kisiwa Cha Mafia...
Uwanja wa ndege wa Mafia...
Nikiweka kumbukumbu ndani tya Mji wa Mafia.
Pipa likiwa limetia timu ndani ya kiwanja kidogo cha ndege cha Kilwa Masoko.
Jengo la Uwanja wa Ndege wa Kilwa Masoko.
Hoteli ya kisasa ndani ya mji wa Kilwa Masoko... maarufu kwa Mzee Sultani
Nangurukuru mjini.
Nangurukuru mjini utakutana na vibao hivi.
Nangurukuru kuna samaki wa kutosha...
Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo akiweka kumbukumbu mbele ya jenngo la halmahauri ya wilaya ya Kilwa.
Ofisi za halmahauri ya wilaya ya Kilwa.