Mgeni rasmi akiwa katika meza kuu na Mkuu wa chuo , pamoja na viongozi wengine wa chuo na viongozi wa Serikali ya wanafunzi
Kutoka kushoto ni Fabian, Dotto Mandolin Kahindi, Abushehe Nondo, Benjamin Mwangoka
Rais Mstaafu wa DASJOSO Alfred Ochali akisoma risala
Mkuu wa Chuo cha DSJ, Joachim Rupepo akitoa hotuba yake na kumkaribisha mgeni rasmi.
Wahitimu wakiwa wanasikiliza kwa umakini hotuba kutoka kwa mgeni rasmi
Kutoka kushoto ni Anifa, Grace, Zourha na Cartace ambao pia walikuwa wahitimu katika mahafali hayo
Wahitimu wakiwa wanatunukiwa akiwemo mwandishi wa habari wa Redio Clouds Fm, Jimmy Jam (wa nne kutoka kulia).
Wahitimu wakiwa wanatoa mkono wa Shukurani baada ya kutunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali Wahitimu wakiwa katika pozi baada ya kumaliza mahafali.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira, Zourha Malisa (anayeongoza msafara mbele) akitoa mkono wa asante kwa mgeni Rasmi, Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari -(DSJ) pamoja na viongozi mbalimbali waliofika katika mahafali hayo ya 19 katika chuo hicho yaliyofanyika Msimbazi Center jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kutoka kushoto ni Elizabeth Lazaro akiwa na Jackline Marandu ambao pia ni wahitimu.
Wageni waalikwa wakiwa wanafuatilia kwa makini kinacho endelea katika mahafali hayo
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira, Zourha Malisa (wa pili kulia) akicheza muziki na wahitimu wenzake wakati wa mahafali ya chuo hicho cha DSJ yaliyofanyika Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakiwa katika nyuso za furaha.
---
---
Mahafali ya 19 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yamefanyika ijumaa ya desemba 13 mwaka huu ambapo wahitimu katika ngazi za stashahada na cheti kwenye fani ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma, na mahuasiano ya umma wamehitimu.