Napenda kuchukua wasaa huu binafsi kuwashukuru wadau wa Blog hii kwa kuiunga mkono japo kwa uchache wao, huku nikiamini kwamba huu ni mwanzo mzuri na huko tuendako tutakuwa wazuri zaidi.
Heri ya Krismas na shukrani sana kwa kuichagua Blog ya Mdimu kila kunapokucha.
lakini shukrani za dhati kwa Kaka Muhidin Issa Michuzi, hajajua tu lakini kaleta ajira na kipato kwa vijana, amechangia vijana wengi sana kujiajiri na kuwa na maisha bora, nikipata nafasi nitamwambia mwenyewe lakini nyie mnaosoma mkimuona mwambie akiweza hata hizi salamu aweke kwenye blogu ya jamii, tunatambua mchango wake na tunamshukuru sana.
Binafsi nina shukrani za dhati kwa Bloggers Cathbert Angelo, Mroki Mroki, Ahmad Michuzi na Othman Michuzi.
Hawa jamaa kila kukicha wananichukulia kama tumezaliwa tumbo moja, sijajua sababu maana hakuna la maana nililowahi kuwafanyia, lakini kila ninapokutana nao hunipa ushirikiano hata wa kutembea, kwa kunishika mkono na kuniambia pa kupita, na wakati mwingine hata kuniuliza kama nimekula au ninataka nini.
Huu ni upendo wa ajabu sana, msinione nimenyamaza nawafikiria sana na cha kuwalipa sina, ila yote kwa yote, nawatakia heri ya sikukuu ya krismas.
Nawapenda sana!