Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

WIVU WA MAPENZI NA UKATILI WA KIJINSIA: MAMA MMOJA AMWAGIWA MAJI YA MOTO MWILI MZIMA

$
0
0
Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa
na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI
KWA PICHA UTAKAZOZIONA

Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili
mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA
UTAKAZOZIONA
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili
mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. SAMAHANI KWA PICHA
UTAKAZOZIONA


 Na Gadiola Emanuel -Arusha


Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha, Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto

katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa
ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa
kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.

Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount
Meru alikolazwa, Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma
lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka
afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa
kumwagia maji ya moto.Neema Teti-Majeruhi



Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini
hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la
madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru
Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo
yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali

nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo
vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini

Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza
wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia
katika hospitali ya mount Meru, amesema yanapotokea matukio
hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza
swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo
hayo.Maria Maswa-Afisa Dawati
la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza
kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa
kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507
zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa. Picha
zote na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles