Wasanii wa Kikundi cha ngoma wakitumbuiza wakati wa Tamasha la mimi ni Afrika,Afrika ni mimi Lile tamasha la kupinga matumizi ya Rushwa na utoaji limefana sana jana Jijini Arusha kwenye viwanja vya general tyre.Kauli mbiu ya tamasha hilo ilikuwa "RUSHWA SIO" na kubebwa na ujumbe mzito wa mimi ni Afrika na Afrika ni mimi.
Dhumuni kubwa la tamasha hilo ilikuwa ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya utoaji na upokeaji rushwa, kiingilio ilikuwa ni bure kabisaaa. Sambamba na elimu iliyotolewa viwanjani hapo pia wakazi wa Jiji la Arusha walipata nafasi ya kupata burudani ya kufa mtu kutoka kwa wasanii kama Izo B, Stamina, Weusi, Chindo man, Roma, Fid Q, Linah, Naziz na Vanessa Mdeee.