Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

HAYAWI HAYAWI SASA UHURU MARATHON DEC 8

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
ZIKIWA zimebaki siku chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kufanyika, tayari wanariadha mbalimbali wameapa kufanyika katika mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.

Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya mbio hizo imepanda, hasa baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa mataifa mbalimbali.

Melleck alisema, mbali na wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha lengo lake.

Mpaka sasa tayari kuna wanariadhaa maarufu waliojiandikisha kutoka Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Ethiopia, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi na Marekani.

Wengine wanatoka Ujerumani, Jamaica, Urusi, China, Japan, Venezuela, Comoro, Nigeria, Italia, Canada, Madagascar na Uturuki.

Mmoja wa wanariadha hao ni bingwa wa dunia wa marathon kwa upande wa wanawake, Edna Kiplagat wa Kenya anayetarajiwa kuwasili nchini Jumamosi.

“Hii ni faraja kubwa kwetu, kwani inaonyesha kwa kiwango kikubwa lengo letu la kupigania amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu linakubalika na watu wengi duniani,” alisema.

Aidha Melleck alisema usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>