Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE wiki hii, nimepata nafasi ya kuzungumza na vijawa
wawili wa kiTanzania wanaosoma nchini China. Nao ni Fatuma Matulanga
aliyeko Beijing na Evans Mhando aliyeko Nanchang ambao kwa pamoja
tumejadili mambo kadhaa na zaidi kuhusu vijana
Wameeleza mengi wakioanisha kijana na maisha ya China na Tanzania ikiwemo
1: TOFAUTI KATI YA KIJANA WA CHINA NA TANZANIA
2:TOFAUTI KATI YA ELIMU YA CHINA NA KWINGINE. Ni kweli kuwa China haifunzi ubunifu na ndio maana wanasifika kwa kuendeleza kuliko kubuni?
3: MALALAMIKO KUWA BIDHAA ZA CHINA HAZINA UBORA, YANATAZAMWA VIPI HUKO CHINA?
4: NI KIPI WANACHOJUA SASA KUHUSU CHINA AMBACHO HAWAKUJUA KABLA HAWAKWENDA CHINA?
5: MABADILIKO YA SERA YA MTOTO MMOJA MNAONA IMEPOKELEWA VIPI HAPO?
6: NI KIPI WANACHOTAMANI KINGETOKA CHINA KWENDA TANZANIA (HASA KATIKA TASNIA YA HABARI?)
Na mengine mengi
Usikose kutembelea mtandao huu siku ya Jumatano ili kusikiliza mahojiano kamili
Ni huyu na Yule ya Mubelwa Bandio wa Jamii Production akihojiana na Fatuma
Matulanga na Evans Mhando, wanahabari wa shirika la utangazaji la
Tanzania (TBC) wanaojiendeleza kielimu nchini China.