Mheshimiwa Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akisoma hotuba yake kwa wadau mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa kijitabu cha MWONGOZO WA KUWASIADIA WANAWAKE WALIOFANYIWA UKATILI kilichoandaliwa na Chama cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC). Hii ni katika mwendelezo wa Kampeni ya Siku 16 za Kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto aliyoizindua hivi Karibuni. Katika picha aliyekaa kushoto kwa Mhe. Kairuki ni Mama Nakazaeli Tenga, Mwenyekiti wa Bodi ya WLAC.
Mama Mama Nakazaeli Tenga, Mwenyekiti wa Bodi ya WLAC akitoa maelezo ya awali kuhusu kijitabu cha MWONGOZO WA KUWASIADIA WANAWAKE WALIOFANYIWA UKATILI huku Mheshimiwa Kairuki (aliyekaa) akifuatilia kwa makini.
Mheshimiwa Kairuki akiwaongoza viongozi wa WLAC na wadau wake katika kuinua kijitabu cha MWONGOZO WA KUWASIADIA WANAWAKE WALIOFANYIWA UKATILI kuashiria uzinduzi rasmi wa kijitabu hicho.