* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.
* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.
* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina sh ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako inahusishwa na tukio hilo.
* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.
* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali. Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa namba moja. Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.
MPE ONYO NA MWENZAKO.