Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ESCURP YAANZA KUTOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI JIJINI DAR

$
0
0
TAASISI ya utafiti wa nchi 12 za Kusini na Mashariki mwa Afrika (ESCURP) kwa kushirikiana na Wizara ya fedha wameandaa mafunzo kwa wajasiriamali 350 kutoka sehemu mbali mbali jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa elimu ya kuendeleza biashara zao.

Mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha jinsi ya kupanua soko la biashara ndani na nje ya nchi, jinsi ya kuwa karibu na benki kwa ajili ya kupata mikopo, pamoja na Elimu ya kufanya biashara zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, katika ukumbi wa shule ya Sheria iliopo jijini Dar es Salaam mkuu wa Taasisi hiyo Ted Maliya Mkono alisema lengo la mafunzo hayo ni pamoja na kutoa elimu hiyo ili wajasiriamali hao waweze kujikwamua na kuendelea katika kazi hiyo.
Mbali na hilo alisema wameamua kutoa mafunzo hayo ambayo yamedhaminiwa na Wizara ya Fedha pamoja na taasisi hiyo ni kuwasaidia kuwapa elimu ya jinsi gani wafanye ili waweze kuendelea na biashara zao, badala ya kurudi nyuma.

"Tumeanzisha mafunzo haya bure kwa wafanya biashara wadogo, ili kuwasaidia kuendelea mbele," alisema Maliyamkono.

Alisema wafanyabiasha wengi wadogo wamekuwa wakifanya biashara zao bila ya kuwa na elimu ya kutosha jinsi ya kuweza kujiendeleza.
Alifafanua zaidi ya kuwa baada ya wao kufanya utafiti waliomba Serikali kupitia Wizara ya fedha, ndipo wakasaidiwa fedha kutoka taasisi hiyo ya Afrika, za kuendesha mafunzo hayo.

Alisema wameanza zoezi hili jijini Dar es Salaam, ambapo litakuwa na siku 10, na baadae watakwenda jijini Mwanza, kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wajasiliamali 150.

Alisema huu ni mwanzo tu, lakini wataendelea kutoa elimu hiyo kila mara katika mikoa mbalimbali ili kusaidia wajasiriamali wa Tanzania kuweza kusonga mbele katika biashara zao.
Naye Haji Dachi, ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo yaliyoanza jana katikia ukumbi wa Shule ya Sheria alisema wahitimu watakaomaliza mafunzo hayo,watakabidhiwa vyeti kwa ajili ya kwenda kuendelea na biashara zao.

Alisema mara baada ya zoezi hilo, (ESCURP) itakuwa ikiwafuatilia wajasiriamali hao ili kujua kama wanayatumia mafunzo waliyoyapata katika siku chache hizo ambazo wamejifunza.

Alisema katika siku hizo wamejipanga kutoa elimu ya kutosha ili kuhakikisha wanapata kile ambacho kitawasaidia katikia ufanyaji biashara zao za kila siku.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>