Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu, Khamis Dakota akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho yao ya miaka minne tokea bendi yao imeanzishwa. Pembeni yake wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’.
Mwanamuziki Khalid Chuma ‘Chokoraa’ (kulia) akitilia jambo mkazo.
Waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo ndani ya kiota cha etasi (zamani Bussines Park) uliopo Victoria jijini Dar.
---
BENDI ya Mapacha Watatu inayoongozwa na wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’ leo Ijumaa Nov 22 katika ukumbi wa letasi (zamani Bussines Park) uliopo Victoria jijini Dar inatarajia kuzindua albam yake ya pili waliyoipa jina la Yarabi Nafsi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja wa bendi hiyo Khamis Dakota alisema kuwa baada ya miaka mine yenye changamoto nyingi wameamua kusherehekea pamoja na wanamuziki wakongwe kutoka bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
Bendi ya Mapacha Watatu ina albamu mbili ambazo ni Shika Ushikacho na Yarabi nafsi.
Dakota akizitaja nyimbo zilizomo katika albamu yao ya pili Yarabi Nafsi ni pamoja na Yarabi Nafsi uliobeba jina la albamu, Ujasiriamali, Naonewa, Chanzo Wanaume, Sumu Ya Mapenzi Remix, Usia wa Babu, Mpenzi Nenda na Wivu.
Naye Khalid Chuma Chokoraa alisema kwamba anawaalika mashabiki wa bendi hiyo waje kwa wingi leo kwani kutakuwa na burudani ya aina yake ambapo wakishuka FM Academia wakiingia Mapacha Watatu kazi itakuwa bubwa.
Akizuungumzia safari ya muziki ya bendi hiyo Meneja Dakota amesema kwamba wamepitia misukosuko mingi, kiingilio ni sh. 10,000.