Mwanamuziki wa kundi la P - Square, Paul Okoye akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarake Nyerere, Tayari kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania, Msanii huyo aliambatana na Pacha wake Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P- Square. Wasanii hao wameambatana na wenzao 13 ambao watatoa burudani jumamosi ya tarehe 23 Novemba. Tamasha hilo limeandaliwa na East African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Wanamuziki wanaotajwa kuwa na mvuto zaidi barani Afrika, P Square, wamewasili usiku huu katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere kwa ajili ya onesho lao linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika viwanja va Leaders Club maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Pichani juu ni Petter(wa pili kutoka kushoto na Paul). Kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East africa Radio na TV
Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao
Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea...
Vijana wakielekea kupumzika tayari kwa kazi.