Hapa anazuia damu sehemu aliyopigwa isindelee kuvuja kwa kutumia kitambaa. |
Baada ya kupata nafuu anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi huyo. |
Hakuishia hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na kumpa kipigovile alivyojiskia ili amalizie hasira zake. |
Kumbuka kipigo hicho kinafanyika mbele ya kituo cha polisi huku kukiwa na ulinzi mkali umeimarishwa. |
Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka! |
BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.
Askari wa kike na wakiume wakimdhibiti kwa bakora na marungu mwanafunzi wa chuo cha IFM (mwenye nguo za blue) baada ya kumchomoa kwenye jengo alilojificha ili kukwepa mabomu ya machozi. |
Mwanafunzi huyu alilala kabisa na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu ya machozi yaliyopigwa kwenye eneo la kituo hicho cha Polisi. |
Mwanafunzi huyu alidondoka kwenye Difenda baada ya Defenda hilo kujazana wanafunzi wengi ambao wakipelekwa kwenye kituo cha Polisi Kigamboni. |
Baada ya kitikisa mabomu yakutosha kwenye baa pembeni ambako walijificha wanafunzi hao walitaka amani itawale huku wakikimbilia gari la polisi ili wajisalimishe. |
Huyu alishikiliwa mapema mara baada ya mabomu kuanza kupigwa, huku akionja joto ya jiwe ya askari hao ambao walionekana kuwa na uchu wakupiga. |
Hapa amri ilikuwa ni mwendo wa kutembea kwa magoti lakini kipigo cha bakora kililazimisha wengine kuwaruka wenzao ama kuwakanyaga wale waliochini. |