Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

JE UNAMFAHAMU MKALI WA SINEMA RAMBO??

$
0
0
Jina lake anaitwa Sylvestar Stallone a.ka. Rambo moja ya mastaa wakubwa kabisa katika sinema za Kimarekani. Miaka mingi iliyopita kabla ya mafanikio yake tunayoyaona leo Rambo aliteseka katika kila kona kwenye kupambana ili atoke kimaisha. Kuna muda ilibidi kuiba vito vya thamani kama hereni na mikufu ya mpenzi wake na kuviuza ili aweze kuyamudu maisha. Mambo yalizidi kumuendea vibaya na ikafika mahali akawa hana hata mahali pa kuishi.

Katika jiji la New York alipokuwa anatafuta maisha ilimbidi kulala kwenye kituo cha mabasi kwa siku tatu akiwa hana hata uwezo wa kujinunulia chakula. Wakati huo alikuwa anamiliki mbwa na aliamua kumuuza mtaani kwa mpita njia yeyote ambaye angekuwa anamtaka kwa kuwa maisha yalikuwa tayari yamemuendea kombo, hakuwa na chakula chake yeye mwenyewe achilia mbali chakula cha kumpa hata huyo mbwa. Baadaye alifanikiwa kumuuza mbwa wake kwa kiasi cha dola 25 (Kama shilingi elfu 40 za kitanzania). Rambo aliondoka analia baada ya kumuuza mbwa ili aweze kujikimu kimaisha.
Wiki mbili baadaye Rambo alihudhuria pambano la ngumi la Mohammed Ali bado maisha yakimwendea vigumu. Baada ya pambano hilo ndipo alipopata wazo la kuandika script za movie maarufu aliyoicheza ya Rocky. Aliandika scripts hizo kwa masaa 20 na kisha kuamua kuiuza kwa wenye studio za kutengeneza sinema kwa dola 125,000 (Zaidi ya shilingi milioni 150 za kitanzania) lakini alikuwa na ombi moja, alitaka yeye pia awepo na ashiriki kucheza sinema hiyo kama Rocky mwenyewe. Wenye studio wakamkatalia. Walitaka kumtafuta star wa kweli, mtu ambaye tayari alikuwa na heshima na jina katika Hollywood ili kucheza sinema hiyo.

Rambo akaamua kutoiuza script yake na akaondoka. Wiki chache baadaye wakamuita na kumuongezea dau lakini kwa sharti lile lile kwamba atakayekuwa star si yeye bali mtu mwingine. Safari hii wakampa dola 250,000 (Zaidi ya milioni mia tatu hamsini za kitanzania). Bado akakataa. Wakaongeza mpaka dola 350,000 (Zaidi ya nusu bilioni za Kitanzania) lakini asiwepo kwenye kucheza movie yenyewe. Walitaka script aliyoandika lakini yeye hawakumtaka. Rambo akagoma kuuza. Alitaka awepo katika ile movie na acheze kama main character (Starring). Baada ya muda ile studio wakakubali acheze kama main character (Starring) na wakamlipa dola 35,000. (Kama milioni 55 za Kitanzania) na Rambo ndipo aliposhiriki katika movie ya Rocky.
Kilichofuata baada ya hapo ni historia. Sinema ya Rocky ilishinda tuzo za Best Picture, Best Directing na Best Film Editing pamoja na tuzo mashuhuri ya Oscar. Rambo mwenyewe aliteuliwa kugombea tuzo ya mwigizaji bora na sinema ya Rocky imeingizwa katika orodha ya sinema bora zaidi kuwahi kuchezwa katika historia ya Marekani.

Unajua kitu cha kwanza kununua na zile dola 35,000 kilikuwa ni nini? Yule mbwa wake. Alisimama kwenye ule mtaa alipomuuzia kwa siku tatu mpaka alipomuona yule aliyemuuzia. Jamaa akakataa kuchukua dola 25 na mwisho Rambo ilibidi akubali kumnunua mbwa aliyemuuza kwa dola 25 kwa dola 15,000.
Leo hii Rambo aliyelala stendi ya mabasi na kushindwa kumudu chakula ni mtu mashuhuri duniani.

Hakuna kitu kibaya kama kuishiwa na kutokuwa na fedha kwenye maisha hasa wakati unazihitaji kufanyia mambo yako. Umewahi kuwa na ndoto? Ndoto ya kufanya kitu kizuri lakini ukashindwa kuitimiza kwa sababu ya umaskini? Mimi nimekuwa na wakati mgumu kama huo mara nyingi kwenye maisha. Mara nyingi sana.

Maisha yana kukata tamaa. Kuna muda utaona nafasi zinakupita. Watu watataka mawazo yako lakini wewe hawatakutaka. Dunia iko rafu. Kama huna utajiri au umaarufu au hauko connected kutakuwa na kukata tamaa kwingi sana. Utaona milango inajifunga ukijiandaa kuingia, watu watakuibia mawazo yako kujitajirisha wao wenyewe. Utajituma na kujituma lakini utaona hakuna mafanikio.
Lakini usiache kuwa na ndoto, kuwa na bidii na kumuamini Mungu! Wapo watakaokubeza kwamba umesoma kazi huna au umri umeenda na maisha yanakushinda, watakuona huna maana, watakuhukumu kwa kila hali. Usipoteze lengo, tazama mbele. Kama bado uko hai story yako bado inaandikwa na chochote kinaweza kutokea. Usiache kuomba na kuamini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles