Sehemu ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa vichwa vipya sita vya treni vya Shirika hilo, leo asubuhi katika stesheni ya TAZARA. Vichwa hivyo sita vimetolewa na Serikali ya China.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Vichwa vipya sita vya treni vya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), katika stesheni ya TAZARA leo Asubuhi. Kushoto kwa Waziri Mwakyembe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka.
Waziri wa Uchukuzi wa Zambia, Yamfwa Mukanga, akitoa hotuba yake kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kabla ya kuzindua vichwa vipya sita, katika stesheni ya TAZARA leo asubuhi.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto), Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Bw. Li Xuhang (katikati) na Waziri wa Uchukuzi wa Zambia, Yamfwa Mukanga(kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa vichwa vipya sita vya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) vilivyotolewa na Serikali ya China, leo asubuhi katika stesheni ya TAZARA.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati), muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania, Bw. Li Xuhang (wa tatu kutoka kwa Waziri Mwakyembe) na Waziri wa Uchukuzi wa Zambia, Yamfwa Mukanga (katikati), wakipeperusha bendera kuashiria kuanza kwa safari kwa vichwa vipya sita vilivyozinduliwa leo katika stehseni ya TAZARA.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akifurahia jambo na Wazazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Na Bi. John Nchimbi, wakati wa uzinduzi wa vichwa sita vipya vya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), vilivyozinduliwa leo Asubuhi, katia stesheni ya TAZARA
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)