Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akishirikiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa kukagua vifaa vya michezo muda mfupi kabla ya Waziri kukabidhiwa rasmi vifaa hivyo vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa. Vifaa hivyo vitatumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom ilikabidhi jezi za soka seti 12, mipira 40 na kombe kubwa la Mshindi
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea kombe kubwa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza wa mashindano maalum kwa shule za sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na Wizara.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Yasoda. Vodacom ilikabidhi pia jezi za soka seti 12 na mipira 40.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangala akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa ajili ya mashindano maalum kwa shule za sekondari za mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na Wizara.
Waandishi wa Habari wakimfuatilia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangala wakati akiongea kwenye hafla ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo kutoka Vodacom vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya shule za Sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na Wizara.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa akifanunua jambo kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangala wakati walipofanya mazungumzo mafupi baada ya hafla ya amkabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano maalum ya shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
---
Vodacom yakabidhi vifaa kwa Waziri Mukangala vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala leo amepokea vifaa vya michezo kutoka Vodacom kwa ajili ya kutumika kwenye mashindano maalum ya sekondari yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar es salaam.
Akipokea vifaa hivyo ambavyo ni jezi seti 12 na mipira 40 pamoja na kombe kwa ajili ya bingwa wa michuano hiyo Waziri Dk Mukangala ameelezea kufurahishwa kwake jinsi ambavyo Vodacom walivyopokea ombi la Wizara la kusaidia mashindano hayo.
Amesema lengo la mashindano hayo ni kuendeleza azima ya serikali ya kutengeneza fursa ya ukuzaji na uendelezaji michezo kwa ngazi za chini kupitia falsafa ya michezo jamii.
“Michezo ni gharama inahitaji fedha nyingi kugharamia vifaa, mafunzo kwa walimu, viwanja na gharama nyengine za uendeshaji ndio maana naipongeza sana Vodacom kwa kukubali ombi letu la kusaidia mashindano haya maalum yatakoyoshirikisha shule 12 za sekondari za Mkoa wa Dar es salaam.”Alisema
“Mashindano haya ni ya majaribio tukiangalia namna ambavyo tunaweza kuwekeza vya kutosha kwenye michezo ngazi ya mashuleni kwa nchi nzima, tutaanza na mchezo wa soka ila mipango ni kupanua wigo kwa kuongeza mpira wa pete na riadha kwa hapo mwakani ikihusiha mikoa mingi zaidi.”Alisema Dk. Mukangala
Waziri Dk. Mukangala amesema Wizara yake inaimani kubwa juu ya mpango huo huku akizitaka jamii kuyapokea na kuyaona kuwa ni sehemu yao ili pamoja na kuyapapa mafanikio bali pia kuwatia moyo watoto wakati wote watakapokuwa waskishiriki.
Amesema kuwa anatambua kuwa mahitaji ni makubwa na kwamba kila shule hapa nchini ingependa kushiriki lakini kwa kuanzia watachagua shule 12 za sekondari kama majaribio huku mipango ikiendelea kuwekwa sawa ili mashindano hayo yawe mapana zaidi kwa hapo mwakani.
“Tuna shule nyingi hapa tu Dar es salaam tumepata wakati mgumu sana kuchagua wawakilishi wa kila Wilaya lakini kwa sasa tunaanza na hizo chache tukiwa na Vodacom na baada ya kumalizika tutafanya tathmini kuona namna ya kuyaongezea wigo wa ushiriki na wa kijiografia.”Alisema Dk. Mukangala
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa amesema Vodacom inatambua umuhimu wa kuwaandaa wachezaji katika ngazi za chini ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya michezo nchini.
“Kukubali kwetu kuwa wadhamini kumesukumwa na imani yetu juu ya maendeleo ya michezo nchini tukiamini katika kuwekeza kwa wanafunzi mashuleni, leo tunafuraha kuwa sehemu ya miapngo ya serikali kukamilisha kile ambacho kila mtu anapenda kukiona kikifanyika katika michezo.”Alisema Twissa
“Tumekuwa wadhamini wa Ligi Kuu Vodacom ambayo imekuwa ikipiga hatua kubwa kimaendeleo hasa kwenye eneo la ushindani hivyo ili mafanikio hayo yawe endelevu ni lazima tuwe na misngi mzuri wa kuzalisha wachezaji wenye ubora na viwango na kwamba njia moja ya msingi ni kuwa na mashindano ya ngazi za chini hasa mashuleni”Alisema Twissa
Amesema vifaa walivyovitoa ni sehemu ya Vodacom kuunga mkono juhudi za serikali za kutekeleza mikakati ya uzalishaji, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na kwamba Vodacom inafurahia mpango huo.
Mashindno hayo maalum yataratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa – BMT na kwamba utaratibu umewekwa wa kuapat sekondari 12 kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es salaam ambapo kila Wilaya itatoa sekondari 4.