Lagos , Septemba 2o , 2013... Timu zote za wavulana na wasichana zimeingia robo fainali katika michuano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanayofanyika Lagos , nchini Nigeria na mshindi atapata medali , kombe pamoja na dola za marekani 10,000.
Timu ya wasichana imetinga robo fainali baada ya ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Malawi jana na kumaliza na pointi nne katika kundi ambapo timu ya Uganda ikishika uskani kwa point sita. Wakicheza kwa kujiami timu ya wasichana ya Tanzania ilipata goli katika dakika ya 17 kupitia kwa mshambuliaji hatari Shelda Boniface , kabla ya Malawi kuzawazisha dakika ya saba katika kipindi cha pili.
Mshambuliaji mwenye uwezo wa hari ya juu Athanas Mdam alionyesha makeke yake jana baada ya kufunga magoli matatu (hat-trick) katika mechi dhidi ya Sierra-Leon ambapo Tanzania ilishinda 4-2 na kukata tiketi ya kushiriki hatua inayofata ya michuano ya Mwaka ya kimataifa inayoandaliwa na Airtel.
Mdamu ambaye amedhiliisha kwamba yeye ni liungo muhimu katika michuano hii , alifunga magoli katika dakika ya 6, 48, 56 , Omari Hamisi ndiye aliitimisha goli la nne la Tanzania katika dakika ya 60. Sierra-Leone walipata magoli yao kupitia kwa Mohamed Mustapha katika dakika ya 8 na Alimamy katika dakika ya 14.
Timu ya wavulana ya Tanzania itacheza mechi ya robo fainali na Madagascar leo wakati wasichana watacheza na Democratic Republic of Congo. Timu ya wavulana itakosa huduma ya mpikaji mabao Athanas Mdamu ambaye yupo majeruhi.
Mshambuliaji hatari Athanas Mdamu ametoa mchango mkubwa sana katika timu mpka kufikia hatua ya mtoano . Amefunga goli kwa kila mechi , dhidi ya Ghana na Zambia. “ Tutamkosa ila tutapigana mpaka mwisho kuakikisha tuanshinda mechi zote.”Alisema naodha wa timu Thomas Chndeka .
Timu nyingine zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwa upande wa wavulana ni mabingwa watetezi Niger ,wenyeji Nigeria , Chad, Malawi, Madagascar, Zambia, na Congo. Na kwa upande wa wasichana ni mabingwa watetezi Ghana , Nigeria , Chad, Kenya , Uganda , Malawi and DRC.
Mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars ni mpango wenye lengo la kuchangia maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika. Pia vijana wanapata fulsa ya kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika medani ya soka.