Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akikabithi Tshirt zitakazotumika katika wiki ya nenda kwa usalama kwa mwaka huu kwa Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga ambapo Airtel, Puma pamoja na Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu. akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti
Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti wakwanza kushoto akifatiwa na mwakilishi wa Be Forward bw Kohei Shibata na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando kwa pamoja wakimkabithi Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga stika za usalama barabarani kwa mwaka huu. Airtel, Puma pamoja na Be Forward ni wadhamini wa wiki ya usalama barabarani kwa mwaka huu
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga akionyesha stika za usalama barabarani kwa mwaka huu mara baada ya kukabithiwa na wadhamini wa wiki ya usalama kwa mwaka huu ambao ni Airtel, Puma pamoja na Be Forward wakishuhudia (kutoka kushoto) mwakilishi wa Be Forward bw Kohei Shibata, Mkurugenzi Mkuu wa Puma Bwana Philippe Carsaleti na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta PUMA na Be Forward kwa pamoja wameungana na baraza la taifa la usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti idadi ya ajali za barabarani nchini.
Kutangazwa kwa ushirikiano huo kumefanyika leo katika makao makuu ya Usalama Barabarani jijini Dar Es Salaam ambapo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga ametangaza wiki ya nenda kwa usalama barabarani ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ya PUMA ENERGY Mkurugenzi Mkuu wa PUMA ENERGY ndugu Philippe Corsaletti alisema “Sisi kama Puma Energy Tanzania tunaamini katika kufanya shughuli zetu za kibiashara katika mazingira ambayo ni salama na yasiyokua na madhara kwa jamii iliyotuzunguka na pasipo kuharibu mazingira. Wajibu huu sio kwa hapa Tanzania peke yake bali ni kila mahali tunapokuwepo duniani.
Suala la kushirikiana na vyombo vya serikali kama Polisi kitengo cha usalama barabarani limekuwepo kwa muda mrefu na bado litaendelea kufanyika tena kwa nguvu na kwa upana zaidi. Katika kuitika mwito wetu wa kuendelea kutoa mchango wetu katika kufanikisha kampeni nzima ya Usalama barabarani, kampuni ya Puma mwaka huu imegharimia vitu mbali kama stiker za ukaguzi, T-shirt na vitabu vya elimu vya usalama barabarani vyote hivi vikiwa vinathamani ya shilingi za Kitanzania milioni 50.
Bado tunazidi kusisitiza kuwa ajali zote zinazuilika na kinachotakiwa ni kila mtu kwa nafasi yake kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua zinazopaswa.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Be Forward bw. Daniel Mtaalam alisema.”tunatoa wito kwa watu wote kushirikiana nasi kufanikisha zoezi hili na nimatumaini yetu msaada huu tunaotoa itasaidia katika kupunguza na kudhibiti ajali zinazotokea barabarini nakusababisha maafa makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla.
Airtel Tanzania kwa mwaka huu imechangia kuchapisha stika, kutoa elimu kwa kwa waendesha Boda Boda , mashindano ya mpira kuhamasisha vijana pamoja na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 500 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na sisi sote”. Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake.