Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akiwasilisha mada ya kwanza juu ya Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano hapa nchini wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) na wasimamizi wa mitandao ya mijadala hapa nchini, iliyoanza rasmi leo na kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Uliopo eneo la Sinza B, jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) na wasimamizi wa mitandao ya mijadala hapa nchini, iliyoanza rasmi leo na kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sekta ya Washangiaji na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) na wasimamizi wa mitandao ya mijadala hapa nchini, iliyoanza rasmi leo na kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wapiga Picha kutoka Vyombo mbali mbali vya habari wakiendelea na zoezi la kuchukua matukio mbali mbali wakati wa Warsha ya siku mbili kwa magazeti tando (Bloggers) na wasimamizi wa mitandao ya mijadala hapa nchini, iliyoanza rasmi leo na kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Uliopo eneo la Sinza B, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Bloggers mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye Warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Uliopo eneo la Sinza B, jijini Dar es Salaam.
---
---
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini wametakiwa kuitumia mitandao hiyo kuelimisha jamii na kuhabarisha badala ya kuitumia kwa kueneza chuki na lugha za matusi yanayoweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema wamiliki wa Blog nchini wanayonafasi kubwa ya kuleta maendeleo kupitia habari na picha wanazoweka kwenye mitandao yao na kuwataka kutumia fursa waliyonayo kuelimisha jamii na kuonya kuwajibishwa kwa watakaobainika kukiuka sheria za uendeshaji wa mitandao hiyo.
Prof. JOHN NKOMA ni Mkurugenzi Mkuu TCRA ambaye amefungua mafunzo ya siku mbili kwa wamiliki wa Blog nchini yaliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwataka wawatumie wataalam mbalimbali waliopo kwenye mafunzo hayo ili kuwawezesha kuongeza ujuzi wa utekelezaji wa majuku yao.
Kwa upande wao wamiliki wa Blog nchini akiwemo JOSEPHAT LUKAZA, MARIAM NDABAGENGA na CATHBERT KAJUNA wamesema mafunzo hayo yatawawezesha kuboresha utekelezaji wa majukumu yao na kuwafikishia habari wananchi wengi na kwa haraka zaidi .