Mfanyakazi wa huduma ya Ezypesa ya Zantel, Aman Said akiwasaidia kusajili laini zao na huduma ya Ezypesa wateja wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ezypesa.
Mfanyakazi wa Zantel, Hassan, akihudumia wateja wapya wa Ezypesa wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo.
---
Kampuni ya simu ya mikononi ya Zantel imezindua kampeni ya mpya ya Ezypesa, ambayo itawawezesha wateja wake waliojisajili na wale watakaojisajili na huduma ya Ezypesa kujishindia pesa taslimu.
Kampeni hiyo ambayo ilianza wiki iliyopita, kwa mtu ambaye hakuwa amejitambulisha kugawa hela bure kwa watu mbalimbali mitaani, imezinduliwa rasmi wiki hii kwa watu mbalimbali kupewa fedha bure.
Akizungumzia kampeni hiyo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni yake imeboresha huduma za Ezypesa na hivyo kuwaomba wateja wa Zantel ambao bado hawajajisajili kujisajili mapema ili kuanza kufurahia huduma hiyo.
‘Pedeshee wa Ezypesa atakuwa akitembelea sehemu tofauti, na ukiwa na laini ya Zantel iliyosajiliwa na Ezypesa utapewa pesa taslimu’ alisisitiza Khan.
Kampeni ya Ezypesa, ambayo pia itaendelea kuwazawadia watu pesa taslimu katika sehemu tofauti watakazokuwa, inawapa wateja wake ofa nyingine kadhaa kama muda wa maongezi, meseji pamoja na vifurushi vya intaneti.
‘Huduma ya Ezypesa sasa imeboreshwa na inapatikana karibia nchi nzima, hivyo tunawakaribisha wateja wetu kujisajijili na kuanza kutumia huduma zetu ili waweze kujipatia ofa mbalimbali’ alisema Khan.
Huduma ya Ezypesa ni moja wapo ya huduma za awali kabisa za kutuma na kupokea pesa ya kampuni ya Zantel ambazo zimekuwa zikipongezwa na wengi kwa usalama na urahisi wake katika kutumia.