Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo, akiongea katika uzinduzia wa program tatu za uzamili katika masuala ya Kompyuta (Computer Application), ‘Software Engeering’ pamoja na Information na Secutiry' uliofanyika katika hoteli ya Holday Inn jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Wajumbe wa baraza la chuo cha Uhasibu, Arusha wakifuatiliakwa makini uzinduzi huo.
Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Galgotias, Profesa Ashok Saxena akielezea masomo yanayatolewa na chuo chao.
Mwakilishi wa mwenyekiti wa Baraza la chuo cha Uhasibu, Dr. Mohammed Arusha akisoma hotuba fupi.
Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA, Bw. Innocent Mungy, akitoa machache wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa progam tatu za uzamili uliofanywa na Chuo cha Uhasibu cha Arusha(IAA) kwa kushirikiana na Chuo cha Galgotias cha nchini India uliofanyika jiji Dar es Salaam.
Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA, Bw. Innocent Mungy (Kati) akikata utepe wa vitabu vyenye mitaa mipya itakayoanza kufundishwa hivi karibuni na Chuo cha Uhasibu cha Arusha(IAA) kwa kushirikiana na Chuo cha Galgotias cha nchini India. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Galgotias, Profesa Ashok Saxena (kulia) na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo pamoja na mshehereshaji wa hafla hiyo.
Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA, Bw. Innocent Mungy, akionyesha wageni vitabu vyenye mitaa mipya itakayoanza kufundishwa hivi karibuni na Chuo cha Uhasibu cha Arusha (IAA) kwa kushirikiana na Chuo cha Galgotias cha nchini India. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Galgotias, Profesa Ashok Saxena (kulia) na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo pamoja na mshehereshaji wa hafla hiyo.
Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA, Bw. Innocent Mungy, akipokea vitabu vya makubaliano kati ya Chuo cha Uhasibu cha Arusha (IAA) na Chuo cha Galgotias cha nchini India ili aweze kuvizindua.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo akipokea kitabu cha makubaliano.
Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Galgotias, Profesa Ashok Saxena akipokea kitabu cha makubaliano.
Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Galgotias, Profesa Ashok Saxena (kulia) na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo wakionyesha mkataba wa makubaliano kwa wageni waalikwa.
Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Galgotias, Profesa Ashok Saxena (kulia) akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo mara baada ya uzinduzi.
---
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitaka vyuo vya elimu ya juu nchini, kuweka utaratibu wa kuipitia mitaala yao hasa katika eneo la mawasiliano ili iweze kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa teknolojia nchini.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Mamlaka hiyo Innocent Mungy, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa progam tatu za uzamili uliofanywa na Chuo cha Uhasibu cha Arusha(IAA) kwa kushirikiana na Chuo cha Galgotias cha nchini India.
Mungy alisema wakati huu Taifa linapozidi kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja za mawasiliano, ni vizuri vyuo vyote na hasa vya elimu ya juu mkaweka mkazo kwa kuhakikisha mnapitia vyema mitaala ya ufundishaji ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia yaliyopo.
“TCRA imekuwa ikitoa udhamini kwa wanafunzi mbalimbali katika fani za teknohama, hii ni kwa lengo la kuwahamasisha zaidi ili waweze kutilia mkazo katika eneo hilo na hivyo kuongeza idadi ya wataalamu nchini” alisema Mungy.
Alisema mamlaka iliweka utaratibu huo kwa kuwashindanisha wanafunzi mbalimbali wanaotuma maombi huku akiutaka uongozi wa vyuo vyote kuwahamasisha wanafunzi wao katika masomo hayo sambamba na kushiriki katika mashindano yao kwa ajili ya kijiinua kitaaluma.
Awali akizungumzia uzinduzi wa program hizo za uzamili katika masuala ya Kompyuta (Computer Application), ‘Software Engeering’ pamoja na Information and Secutiry' Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo, alisema malengo ya chuo ni kuongeza idadi ya wataalam katika fani hizo ili kuleta ushindani kimataifa.
Alisema kwa ushirikiano kati ya Chuo hicho pamoja na Chuo cha Galgotias cha India, wana imani watu wengi zaidi watajitokeza na kujiunga na masomo ukizingatia pia chuo hicho kimeanzisha utaratibu wa ufundishaji wa masomo kwa muda wa jioni.
Alisema kuanzishwa kwa utaratibu huo wa masomo ya jioni, kumelenga kuhakikisha watu wanaotaka kujiunga na masomo ambao tayari ni waajiriwa wanapata fursa hiyo kwa lengo la kujiongezea elimu huku akiwataka waajiri kuwajli waanyakazi wao kwa kuwadhamini kimasomo.