Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI YA MAKUMBUSHO JIJII DAR, AWA MKALI KWA WAZAZI WASIOWAJALI WATOTO WAO

$
0
0
Wazazi walioitikia wito wa kikao hicho.
Mwalimu Agostino akizungumzia jambo linalowafanya watoto kutojua kusoma wala kuandika shuleni hapo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makumbusho, mwalimu Lyimo akizungumza na wazazi katika kikao cha kujadili maendeleo ya wanafunzi shuleni hapo.
---
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi makumbusho jijini Dar Mwalimu Lyimo leo aliitisha kikao cha kujadili maendeleo ya wanafunzi shuleni hapo na hasa wale wasiojua kusoma na kuandika. Hii ni katika mikakati aliyojiwekea kwa kufanya mikutano ya wazazi na walimu wa madarasa mara kwa mara kujadili maendeleo ya mwanafunzi shuleni hapo.

Mwalimu Lyimo alilaani vikali vitendo vya baadhi ya wanafunzi kutojua kabisa kusoma na pindi wazazi wanapoitwa kutotoa ushirikiano, kuhusiana na hilo ameahidi mwakani kutopokea mwanafunzi wa darasa la kwanza asiyepitia shule za awali(chekechea) na atawatimua wale wanafunzi wasiokuwa na maendeleo mazuri na wazazi hawataonesha ushirikiano.

Wakati huohuo katika kikao hicho baadhi ya wazazi walilalamikia walimu kutokuwa makini madarasani na kuwalazimisha watoto wabaki tuisheni, na kupelekea wale watoto wasiosoma tuisheni kukosa masomo kamilifu kwani masomo yote hufundishwa zaidi tuisheni na sio madarasani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>