Ni masikitiko makubwa kwa wanafunzi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dodoma kwa kumpoteza mwanafunzi mwenzao Bi. Restuta Mayuma (pichani) ambaye alifariki tarehe 05/08/2013 (Jumatatu) mnamo mishale ya saa kumi na moja jioni.
Hata hivyo mwanafunzi huyo alikuja dodoma kwa lengo la kufaya mitihani yake ( katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wa Chuo cha CBE wamekuwa wakiendelea kufanya mitihani yao ya Special pamoja na ile ya Supplimentary.
Marehemu Restuta, Alikuwa anasoma Diploma, kozi ya Uhasibu (Accountancy), ambapo alianza masomo ya Diploma mwaka wa masomo 2011/2012 na alitakiwa kuhitimu Elimu yake ya Diploma mwaka 2012/213. Lakini kwa kipindi hiki alikuja chuo kurudia mitihani yake ya Diploma I.
Akizungumza na blog hii Rafiki wa karibu sana na Mwanafunzi huyo (Marehemu Restuta) alisema Marehemu alikuwa anasumbuliwa na homa za hapa na pale (Malaria) hali ambayo ilipelekea mpaka kutokea kwa kifo chake.
Tayari Mwili wake umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Dar es salaam eneo la BUNJU kwa ajili ya shughuli za Mazishi ambapo mwili huo umesafirishwa na Gari la Chuo (CBE) Kwa kuambatana na WARDEN, Mashauri Machunde (Mwanafunzi CBE) pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu waliokuwepo mkoani Dodoma.
Akizungumza kwa njia ya simu, Bw. Mashauri Machunde (Mwanafunzi CBE) amewataka wanafunzi wote wa CBE wanaoishi jijini Dar es salaam kijitokeza katika mazishi ya Mwanafunzi huyo yanayotarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwao "Bunju " Kwa kupanda magari yaendayo Bunju na kushukia eneo la Bunju "A" kituo kinaitwa Shule au Hospital (Uliza kwa Mzee Mayuma karibu na Shule ya Sekondari Fanaka).