Mkuu wa Mkoa wa Singida akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Uchukuzi, wakati alipotembelea mabanda ya Wizara hiyo na Taasisi zake katika maonesho ya kitaifa ya kilimo yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma. Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Zalisha mazao ya kilimo na Mifugo kwa kulenga mahitaji ya Soko'.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Parseko V. Kone (mwenye suti nyeusi) akisisitiza jambo kwa Afisa Mwandamizi wa Masoko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bi. Lydia Mallya (kulia), wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika maonesho ya kilimo katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Betty Mkwasa akiangalia mfano wa mabasi ambayo yatatumika kwa ajili ya usafiri wa abiria jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini(SUMATRA) katika viwanja vya maonesho ya kilimo nanenane mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Parseko V. Kone.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)