Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ASKARI POLISI BADO WANAHITAJI ELIMU JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA SIRAHA ZA MOTO WANAZOZITUMIA

$
0
0
 Jana majira ya saa nane mchana katika eneo la Tabata Relini kamera ya Kajunason Blog ilishuhudia kitendo ambacho si cha kiungwana cha askari polisi kufika eneo la kazi ya mtu na kumkamata huku wakipiga mabomu ya moto kuwatishia wananchi. Hakina nilijikuta nikisema, 'ASKARI POLISI BADO WANAHITAJI ELIMU JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA SIRAHA ZA MOTO WANAZIZITUMIA' namshukuru Mungu nilipofika eneo la tukio na kuona mwandishi wa habari waliweza kuondoka haraka eneo la tukio jambo ambao lilionyesha walichokuwa wanakifanya si sahihi. Vile vile nilimnasa askari mmoja akipiga ovyo siraha ya moto kama kuwatawanya wananchi jambo ambao kiukweli hakukuwa na ulazima wa kupiga kwa vile wananchi walikuwa kimya.
 Askari Polisi akiweka bomu kwenye siraha yake.
 akiweka sawa siraha yake...
 akijiweka sawa kufyatua risasi.
 akifyatua risasi ya moto, jambo la kujiuliza  je risasi hiyo inapompata mtu si anakufa kana alivyouwawa mwandishi Mwangosi wa Iringa??? Ombi langu kwa Jeshi la Polisi nchini ni vyema kuwapa mafunzo ya utumiaji wa vyombo hivi ambavyo wakati mwingine havina ulazima wa kutumika maeneo ya wananchi. Vile vile waweze kuangalia na askari wa kuwakabidhi maana vijana wengi wao huona ufahari kufyatua ovyo risasi jambo ambao kiukweli ni harati kwa maisha ya watu.
 Hapa wakiwa wamemkamata kijana ambaye walikuwa wakimtuhumu kuwa ni kibaka.
 Hapa wakijaribu kuondoka eneo la tukio baada ya kuona kamera ya Kajunason Blog imefika kunyaka tukio.
 Ukiangalia askari polisi aivyoshika siraha yake licha ya kutoangalia usama wa wenzake.
 Akipanda kwenye gari huku silaha yake akiwa amewaelekezea wenzake jambo ambalo ni hatari.
 Wananchi waliokuwa wamejitokeza eneo la tukio.
 Hapa askari huyo akiikoki siraha yake ambayo alikuwa akiipiga kuwatishia wananchi.
Askari hao wakiondoka eneo la tukio huku wakipiga ovyo risasi juu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles